29. Sema kama alivyosema Mtume kuhusu kuonekana kwa Allaah Aakhirah

Imaam Ibn Abiy Daawuud (Rahimahu Allaah) amesema:

وقد يُنكِر الجهمي هذا وعندنا

08 – Kwa hakika kabisa Jahmiy atayapinga haya, na kwetu sisi tuko

بمصداقِ ما قلنا حديثٌ مصرحُ

   kwa usadikisho wa yale tunayoyasema tuna Hadiyth inayotamka wazi

رواه جريرٌ عن مقالِ مُحمدٍ

09 – Jariyr amepokea kutoka katika maneno ya Muhammad

فقلُ مِثل ما قد قال في ذاك تنْجحُ

       sema mfano wa aliyoyasema kuhusu hayo utafaulu

MAELEZO

Mtu Jahmiy atapinga Kuonekana kwa Allaah (´Azza wa Jall) Aakhirah. Hawana mashiko yoyote kwa hayo. Kuhusu sisi katika kuthibitisha Kuonekana tuna Hadiyth nyingi zilizopokelewa kwa njia nyingi kutoka kwa kundi kubwa la Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amezipokea katika “Haadi al-Arwaah ilaa Bilaad-il-Afraah”. Ni kitabu kinachozungumzia Pepo, kimeisifu na kuelezea yaliyomo ndani yake. Ndani yake ametaja Kuonekana kwa Allaah na amesimulia vilevile Hadiyth zilizothibiti kwa mapokezi mengi kwa mtiririko wake, mlolongo wa wapokezi wake na wapokezi wake.

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“Jariyr… “

Anaitwa Jariyr bin ´Abdillaah al-Bajaliy (Radhiya Allaahu ´anh). Ni mmoja miongoni mwa wasimulizi katika Maswahabah. Vinginevyo kuna Maswahabah wengine waliopokea. Amechotaka mtunzi (Rahimahu Allaah) ni kupigia mfano peke yake.

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“… kutoka katika maneno ya Muhammad.”

Bi maana Jariyr alipokea kutoka katika maneno ya Mtume wa Allaah Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“Sema mfano wa aliyoyasema kuhusu hayo utafaulu.”

Bi maana sema kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) utafaulu. Usiende kinyume na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ukaja kula khasara. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hatamki kwa matamanio yake:

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ

“Wala hatamki kwa matamanio. Hayo ayasemayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa kwake.” (53:03-04)

Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni haki na hayaingiliwi na shaka yoyote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 88-89
  • Imechapishwa: 09/01/2024