29. Matahadharisho ya kusoma kwa lengo jengine lisilokuwa ´ibaadah

119 – Abu Sa´iyd Muhammad bin Muusa bin al-Fadhwl as-Swayrafiy ametukhabarisha huko Naysaabuur: Abul-´Abbaas Muhammad bin Ya´quub al-Aswamm ametuhadithia: al-´Abbaas bin al-Waliyd bin Maziyd al-Bayruutiy ametukhabarisha: Baba yangu amenikhabarisha: al-Awzaa´iy ametukhabarisha na akasema:

”Nimezinduliwa ya kwamba ilikuwa inasemwa ´Ole wa ambaye anajifunza kwa lengo lisilokuwa la kufanya ´ibaadah na wale wanaohalalisha mambo ya haramu kwa mambo yenye kutia shaka`.”

120 – al-Hasan bin ´Aliy al-Jawhariy amenikhabarisha: Muhammad bin al-´Abbaas al-Khazzaaz ametukhabarisha: Yahyaa bin Muhammad bin Swaa´id ametukhabarisha: al-Husayn bin al-Hasan al-Marwaziy ametukhabarisha: Ibn-ul-Mubaarak ametuzindua: Bakkaar bin ´Abdillaah ametuzindua: Nimemsikia Wahb bin Munabbih akisema:

”Allaah (Ta´ala) amesema wakati alipokuwa akiwasimanga marabi wa wana wa israaiyl: ”Je, mnajifunza kwa lengo jengine lisilokuwa la dini? Je, mnasoma kwa lengo jengine lisilokuwa la kufanya matendo? Mnaiuza dunia kwa sababu ya Aakhirah? Mnajivisha vazi la pamba na huku mnaficha vazi la mbwa mwitu? Mnaondosha uchafu kwenye vinywaji vyenu na mnameza mfano wa milima ya mambo ya haramu. Mnawatwisha watu dini mfano wa milima na hamnyanyui hata kidole kidogo kwa ajili ya kuwasaidia. Mnarefusha swalah na kuvaa mavazi meupe na wakati huohuo mnapora mali ya mayatima na ya wajane. Ninaapa kwa utukufu Wangu kwamba nitawapiga kwa mtihani ambao utampotosha kila mwenye uoni wa ndani na mwenye hekima.”

121 – al-Hasan bin Abiy Bakr ametukhabarisha: ´Uthmaan bin Ahmad ad-Daqqaaq ametukhabarisha: al-Hasan bin Sallaam ametukhabarisha: Abu Nu´aym ametukhabarisha: Abul-Jaabiyah al-Farraa’ ametukhabarisha: ash-Sha´biy amesema:

”Sisi sio wanazuoni. Lakini tumezisikia Hadiyth na tukazisimulia. Wanazuoni ni wale ambao wanapojifunza wanafanya vitendo.”

122 – al-Hasan bin Muhammad al-Khallaal ametuhadithia: ´Umar bin Ahmad al-Waa´idhw ametuhadithia: ´Abdullaah bin Muhammad bin Ziyaad ametukhabarisha: al-´Abbaas bin al-Waliyd bin Maziyd ametukhabarisha: Baba yangu ametukhabarisha: Nimemsikia al-Awzaa´iy akisema:

”Pindi Allaah anapowatakia watu shari, basi huwafungulia mlango wa mabishano na akawazuilia kufanya matendo.”

123 – Abu ´Abdillaah al-Husayn bin Ja´far as-Salamaasiy ametukhabarisha: Ahmad bin Ibraahiym bin Shaadhaan ametukhabarisha: Ahmad bin Muhammad bin ´Abdil-Kariym al-Wasaawisiy ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Khubayq ametuhadithia: Nimemsikia Ibraahiym al-Bakkaa´ akisema: Nimemsikia Ma´ruuf bin Fayruuz al-Karkhiy akisema:

”Pindi Allaah anapowatakia watu mema, basi huwafungulia mlango wa kutenda matendo na akawafungia mlango wa mabishano. Na pindi Allaah anapowatakia watu shari, basi huwafungulia mlango wa mabishano na akawazuilia kufanya matendo.”

124 – Abul-Qaasim ´Ubaydullaah bin ´Umar bin Ahmad al-Waa´idhw ametukhabarisha: Baba yangu amenihadithia: ´Aliy bin Muhammad al-Miswriy ametukhabarisha: Muhammad bin Zaydaan bin Swuwayd ametukhabarisha: Abu Nu´aym al-Fadhwl bin Dukayn ametukhabarisha:

”Niliingia kwa Zufar wakati alipokuwa katika hali ya kukata roho. Akasema: ”Ee Abu Nu´aym! Natamani yale tuliokuwa tukijishughulisha nayo ilikuwa ni kumtukuza Allaah.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 78-80
  • Imechapishwa: 21/05/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy