29. Je, kuna tofauti kati ya kutenzwa nguvu juu ya ukafiri katika maneno na vitendo?

Swali 29: Kuna watu wanaofanya tofauti kati ya kulazimishwa kwa maneno na kulazimishwa kwa vitendo na wanasema kwamba Aayah inahusu kutenzwa nguvu kwa maneno tu, lakini kwamba hakuna kulazimishwa inapokuja katika matendo?

Jibu: Sahihi ni kwamba hakuna tofauti kati ya hayo mawili muda wa kuwa kulazimishwa ni kwa njia ya dharurah ambayo mtu hana khiyari nayo. Mfano ni pale dhalimu anapoweka upanga shingoni mwake na kumwambia asujudie sanamu na vinginevyo anamuua. Hata hivyo yule anayelazimishwa kwa vitendo anapaswa kuwa na nia ya kujikurubisha kwa Allaah kupitia kitendo chake. Kwa mfano akilazimishwa kusujudia sanamu, basi awe na nia ya kusujudu kwa ajili ya Allaah, kwa sababu wao hawawezi kumiliki moyo wake na sura itaonekana kuwa ni ya kusujudia sanamu lakini moyo wake umetulia kwa imani. Kwa maana nyingine kitendo chake hakitomdhuru.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 65
  • Imechapishwa: 09/01/2026