Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:
14 – Amepokea tena (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule asiyeacha maneno ya uongo, kuyatendea kazi na ujinga, basi Allaah hana haja kwa yeye kuacha chakula na kinywaji chake.”[1]
Hadiyth ni dalili kwamba ni lazima kwa mwenye kufunga kulinda swawm yake kutokana na mambo yanayoathiri na kupunguza thawabu zake, kwa kujipamba na tabia njema na kujiepusha na tabia mbaya kama kusema uongo, kufanya vitendo vyake na ujinga, kwani tabia hizi – ingawa zimekatazwa kila wakati – uovu wake huzidi wakati wa kufunga. Kwa sababu hii zimezungumzwa kuhusu kufunga na kutokea kwake kwa mwenye kufunga kunadokeza kwamba swawm yake ni yenye mapungufu kwa maana na malipo yake ni machache, kwa sababu siyo swawm kamili kikamilifu. Kwani lau ingekuwa hivyo angeilinda swawm yake kutokana na maneno yaliyokatazwa na matendo mabaya.
Hakika wakati wa mwenye kufunga ni wenye thamani na bora zaidi kuliko kutumia kwenye maangamizi haya yanayoathiri malipo ya swawm au kuondoa uhalisia wake na kufuta athari zake za kimalezi na kitabia. Kwa sababu kauli yake
”… basi Allaah hana haja kwa yeye kuacha chakula na kinywaji chake.”
yanaleta hisia kwamba inakhofiwa kwa yule anayefanya kitu chochote kati ya hayo akiwa na swawm yake kwamba swawm yake haikubaliwi.
Hapa kuna dalili kwamba swawm siyo tu kujizuia na vitu vinavyoharibu swawm kihisia, bali lazima pia iwe ni swawm ya viungo vyote dhidi ya yale aliyoyaharamisha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), kujipamba na tabia njema na sifa tukufu ili swawm itimize jukumu lake la kulea nafsi na kurekebisha maadili. Aidha wanaostahiki zaidi hilo ni wale wenye mahusiano na wengine, kama vile hakimu, mwalimu, mwanafunzi, mfanyakazi na mfano wao.
[1] al-Bukhaariy (1903) na Abu Daawuud (2362).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/38-39)
- Imechapishwa: 12/02/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)