95- Kutembea kwa haraka kutoka ´Arafah kwenda Muzdalifah.

96- Kuoga kwa ajili ya kulala Muzdalifah.

97- Kupendelea kushuka kipando ili kuingia Muzdalifah kwa kutembea kwa miguu kwa ajili ya kuiheshimisha Haram.

98- Mtu kulazimiana na du´aa ifuatayo wakati anapofika Muzdalifah:

اللهم إن هذه مزدلفة جمعت فيها ألسنة مختلفة نسألك حوائج مؤتنفة

“Ee Allaah! Hii ni Muzdalifah ambayo imekusanya lugha mbalimbali. Tunakuomba mahitajio yetu… “

Haya yametajwa katika “al-Ihyaa´”.

99- Kuacha kuharakisha kuswali Maghrib punde tu mtu anapofika Muzdalifah na badala yake akajishughulisha na kuokota mawe.

100- Kuswali sunnah ya Maghrib baina ya Maghrib na ´Ishaa au kuzikusanya na sunnah ya ´Ishaa na ya Witr baada swalah mbili za faradhi. Haya yamesemwa na al-Ghazaaliy.

101- Kumulika mataa zaidi usiku wa kuamkia siku ya Nahr katika vituo vya mahujaji Muzdalifah.

102- Kukesha usiku huu.

103- Kusimama Muzdalifah pasi na kulala hapo.

104- Kulazimiana na du´aa ifuatayo pindi mtu anapomaliza kubaki kwake katika vituo vya mahujaji hapo Muzdalifah:

اللهم بحق المشعر الحرام والبيت الحرام والركن والمقام أبلغ روح محمد منا التحية والسلام وأدخلنا دار السلام يا ذا الجلال والإكرام

“Ee Allaah! Naapa kwa haki ya vituo vya mahujaji, nyumba Takatifu, nguzo na sehemu pa kusimama [Ibraahiym]! Ifikishie roho ya Muhammad salamu kutoka kwetu. Tuingize Nyumba ya amani. Ee Mwenye utukufu na ukarimu.”[1]

105- Maneno ya al-Baajuuriy (318):

“Ni Sunnah kukusanya mawe saba Muzdalifah ambayo atarusha siku ya Nahr. Mawe mengine yaliyobaki atayorusha ayaokote kutoka katika bonde la Muhassir.”

[1] Du´aa hii, pamoja na kuwa ni jambo lililozuliwa, ndani yake yako mambo yanayopingana na Sunnah. Nayo ni kufanya Tawassul kwa Allaah kwa haki ya kwa haki ya vituo vya mahujaji na nyumba Takatifu… Inatakiwa kufanya Tawassul kwa Allaah (Ta´ala) kwa majina na sifa Zake. Hanafiyyah wamesema kuwa inachukizwa kusema:

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kwa haki ya vituo vya mahuhaji… “

Haya yametajwa katika “Haashiyah Ibn ´Aabidiyn”. Pia tazama kitabu chetu ”at-Tawassul; Anwaa´uh wa Ahkaamuh”.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah, uk. 53
  • Imechapishwa: 22/07/2018