Hata hivyo mara nyingine hutaja simulizi zao kutoka kwa watu wa Kitabu, ambazo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliziruhusu pale aliposema:
“Fikisheni kutoka kwangu ijapo Aayah moja. Simulieni kutoka kwa wana wa israaiyl na hapana vibaya. Yeyote anayenizulia uwongo kwa makusudi basi ajitayarishie makazi yake Motoni.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr.
Kwa sababu hiyo ´Abdullaah bin ´Amr alipata vitabu viwili vya watu wa Kitabu baada ya vita vya Yarmuuk. Hivyo akawa anasimulia kutoka humo kwa ufahamu wake kutokana na ruhusa hiyo. Lakini simulizi hizi za kiisraaiyl hutajwa kwa lengo la kutilia nguvu na si katika mambo ya ´Aqiydah. Zinagawanyika katika sampuli tatu:
1 – Zile ambazo tunajua kuwa ni sahihi ambazo zinaafikiana na dini yetu na hivyo yakathibiti. Hayo ni sahihi.
2 – Zile ambazo tunajua kuwa ni za uwongo ambazo zinapingana na dini yetu.
3 – Zile zilizonyamaziwa, kwa maana ya kwamba si katika aina ya kwanza wala aina ya pili. Sampuli hii hatutakiwi kuziamini wala kuzikadhibisha, hata hivyo inafaa kuzisimulia kama tulivotangulia kusema. Mara nyingi aina hii haina faida ya dini yetu.
[1] Ahmad (2/159, 202 na 214), al-Bukhaariy (3461) na at-Tirmidhiy (2669).
- Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 90-91
- Imechapishwa: 08/04/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)