Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

1- Allaah (Ta´ala) amesema:

فَإِذَا جَاءَتْهُمُ الْحَسَنَةُ قَالُوا لَنَا هَـٰذِهِ ۖ وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ يَطَّيَّرُوا بِمُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُ ۗ أَلَا إِنَّمَا طَائِرُهُمْ عِندَ اللَّـهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ

”Basi yalipowajia mazuri husema: “Hili letu” na pindi likiwapata ovu hunasibisha nuksi kwa Muusa na walio pamoja naye. Tanabahi!  Hakika nuksi yao iko kwa Allaah lakini wengi wao hawatambui.” (al-A´raaf 07:131)

2- Allaah (Ta´ala) amesema vilevile:

قَالُوا طَائِرُكُمْ مَعَكُمْ أَئِن ذُكِّرْتُم بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ مُّسْرِفُونَ

“Wakasema: “Mkosi wenu uko pamoja nanyi. Je, [mnatutisha] kwa vile mnakumbushwa? Bali nyinyi ni watu wapindukao mipaka!” (Yaasin 36:19)

3- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna maambukizi, kuamini mkosi wa ndege, bundi wala Swafar.”[1]

Ameipokea na al-Bukhaariy na Muslim ambaye ameipokea kwa nyongeza:

 “… na wala hakuna imani fulani kwa kuchomoza kwa nyota au sayari[2] na wala mzimu.”[3]

4- al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutoka kwa Anas ambaye amesimulia kwamba amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Hakuna maambukizi wala kuamini mkosi wa ndege. Inanipendeza al-Fa´l.” Akaulizwa: “Na ni nini al-Fa´l?” Akasema: “Ni neno zuri.”[4]

5- Abu Daawuud amepokea kwa cheni ya wapokezi nzuri ya kwamba ´Uqbah bin ´Aamir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitajiwa mkosi wa ndege kisha akasema: “Nzuri yake ni al-Fa´l. [Ndege] isimrudishe nyuma muislamu. Mmoja wenu anapoona yanayomchukiza basi na aseme:

اللهم لا يأتي بالحسنات إلا أنت ، ولا يدفع السيئات إلا أنت ، ولا حول ولا قوة إلا بك

“Ee Allaah! Nakuna awezaye kuleta mambo mema isipokuwa Wewe na hakuna awezaye kuzuia mambo mabaya isipokuwa Wewe na wala hakuna njia na namna wala nguvu isipokuwa zitokane Nawe.”[5]

6- Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kuamini mkosi wa ndege ni shirki, kuamini mkosi wa ndege ni shirki. Wala hakuna yeyote miongoni mwetu asiyehisi hilo, lakini Allaah huuondosha kwa utegemezi.[6]

Ameipokea Abu Daawuud na at-Tirmidhiy ambaye ameisahihisha na kwamba kipande cha maneno ya mwisho ni ya Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh).

7- Ahmad amepokea kupitia kwa Ibn ´Amr:

“Yule ambaye kutokana na kuamini mkosi wa ndege kukamfanya akarudi nyuma na asiifanye haja yake basi ameshirikisha.” Wakasema: “Ni ipi kafara ya hilo?” Akasema:  “Ni kusema:

اللهم لا خير إلا خيرك و لا طير إلا طيرك و لا إله غيرك

“Ee Allaah! Hakuna kheri isipokuwa ile inayotokamana  na kheri Yako, wala hakuna kuamini mkosi isipokuwa kume kumetokamana Nawe na wala hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe.”[7]

8- Amepokea vilevile kupitia kwa al-Fadhwl bin ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

“Kuamini mkosi ni kule kukufanyako ufanye kitu fulani au kukurudishe nyuma [usifanye kitu fulani].”[8]

MAELEZO

Maelezo hayakuja katika kitabu.

[1] al-Bukhaariy (5757) na Muslim (2220).

[2] Muslim (2220).

[3] Muslim (2222).

[4] al-Bukhaariy (5776) na Muslim (2224).

[5] Abu Daawuud (3919), Ibn Abiy Shaybah (26392) na al-Bayhaqiy (16298). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (843).

[6] Abu Daawuud (3910), at-Tirmidhiy (1614), Ibn Maajah (3538) na Ahmad (3687). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (2850).

[7] Ahmad (7045). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Iswlaah-ul-Masaajid” (1/116).

[8] Ahmad (1824). Cheni ya wapokezi wake ni dhaifu kwa mujibu wa Shu´ayb al-Arnaa’uut.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 99
  • Imechapishwa: 17/10/2018