Mizani ina vitanga viwili ambapo matendo yatapimwa ndani yake. Dalili ni ile Hadiyth juu ya madaftari. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) atamueleza mja juu ya matendo yake na kumuonesha hayo. Kisha kusemwe:
“Je, una matendo yoyote? Una mema yoyote?” Atasema: “Hapana, ee Mola Wangu.” Kisha atasema: “Ndio, una kitendo kizuri kwetu. Mola Wako hamdhulumu yeyote.” Kisha kuwekwe “hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah” kwenye kitanga kimoja cha mzani na madaftari tisini na tisa yawekwe kwenye kitanga kingine cha mzani na “hakuna mungu mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah” iyashinde uzito. Kwa sababu hakuna chenye uzito pamoja na jina la Allaah.”[1]
Katika Hadiyth nyingine imekuja:
“Muusa! Mbingu saba na wakazi wake mbali na Mimi na ardhi saba vikiwekwa kwenye kitanga kimoja cha mzani na “hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah” ikawekwa kwenye kitanga kingine cha mzani, basi “hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah” itakuwa na uzito zaidi.”[2]
Mizani imethibiti katika Qur-aan na Sunnah:
وَنَضَعُ الْمَوَازِينَ الْقِسْطَ لِيَوْمِ الْقِيَامَةِ فَلَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا ۖ وَإِن كَانَ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ أَتَيْنَا بِهَا ۗ وَكَفَىٰ بِنَا حَاسِبِينَ
“Tutaweka mizani za uadilifu siku ya Qiyaamah basi nafsi haitodhulumiwa kitu chochote. [Kila kitu] japo ikiwa uzito wa mbegu ya hardali, Tutaileta. Inatosheleza Kwetu kuwa Wenye kuhesabu.”[3]
وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ
“… na yule ambaye mizani [ya matendo] yake [mema] itakuwa khafifu, basi hao ni ambao wamekhasirika nafsi zao; Motoni ni wenye kudumu.”[4]
فَأَمَّا مَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُمُّهُ هَاوِيَةٌ
“Basi yule itakayekuwa mizani [ya matendo] yake [mema] nzito, huyo atakuwa katika maisha ya kuridhisha, na yule itakayekuwa mizani yake khafifu, basi makazi yake ni Haawiyah.”[5]
[1] at-Tirmidhiy (2639) na Ibn Maajah (4300). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy. Ahmad Shaakir amesema: ”Mlolongo wa wapokezi wake ni Swahiyh.”
[2] Ibn Hibbaan (2324) na al-Haakim (1/528) ambaye ameisahihisha na adh-Dhahabiy ameafikiana naye.
[3] 21:47
[4] 23:103
[5] 101:06-09
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 391-392
- Imechapishwa: 26/08/2017

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 391-392
Imechapishwa: 26/08/2017
https://firqatunnajia.com/28-mizani-imethibiti-katika-qur-aan-na-sunnah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)