Kuna sampuli mbili ya matendo yenye kukubaliwa:
1 – Ni kwamba mja aswali na kufanya ´ibaadah nyingine zote hali ya kuwa moyo wake unashikamana na Allaah (´Azza wa Jall) hali ya kumtaja Allaah (´Azza wa Jall) daima. Matendo ya mja huyu hupelekwa mbele ya Allaah (´Azza wa Jall) hadi yasimame mbele Yake kisha Allaah (´Azza wa Jall) huzitazama. Anapozitazama huzikuta zimetakasika kwa ajili ya uso Wake, zimekubaliwa, zimetoka kwenye moyo ulio salama, mwaminifu na unaopenda kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall) na ukijitokeza kumkaribia. Basi Allaah huyapenda, huyaridhia na huyakubali.
2 – Mja hufanya matendo kimazoea na katika hali ya kughafilika, lakini ananuia kwayo utiifu na kujikurubisha kwa Allaah. Viungo vyake vinashughulika na utiifu lakini moyo wake umesahau kumtaja Allaah. Hivyo ndivyo ilivyo kwa matendo yake yote. Basi yanapoinuliwa matendo ya huyu kwa Allaah (´Azza wa Jall) hayasimami mbele Yake wala haangalii kwake, bali huwekwa mahala pa kuwekwa majalada ya matendo hadi yatawasilishwa kwake siku ya Qiyaamah. Hapo yatatofautishwa; Atamlipa kwa yale yaliyokuwa kwa ajili Yake na kumrudishia yale ambayo hayakuwa kwa ajili ya uso Wake. Kupewa thawabu juu ya matendo hayo ni kumlipa mja kupitia kiumbe miongoni mwa viumbe Wake, kama majumba, chakula, vinywaji na wake wa Peponi. Lakini thawabu ya yule wa mwanzo ni ridhaa juu ya matendo yenyewe, radhi ya Allaah juu ya mja huyo, kumkaribia kwake na kuinuliwa daraja yake na cheo chake. Huyu hulipwa thawabu bila hesabu. Kwa hiyo kuna tofauti kati ya mtu wa kwanza na mtu wa pili.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 48-49
- Imechapishwa: 06/08/2025
Kuna sampuli mbili ya matendo yenye kukubaliwa:
1 – Ni kwamba mja aswali na kufanya ´ibaadah nyingine zote hali ya kuwa moyo wake unashikamana na Allaah (´Azza wa Jall) hali ya kumtaja Allaah (´Azza wa Jall) daima. Matendo ya mja huyu hupelekwa mbele ya Allaah (´Azza wa Jall) hadi yasimame mbele Yake kisha Allaah (´Azza wa Jall) huzitazama. Anapozitazama huzikuta zimetakasika kwa ajili ya uso Wake, zimekubaliwa, zimetoka kwenye moyo ulio salama, mwaminifu na unaopenda kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall) na ukijitokeza kumkaribia. Basi Allaah huyapenda, huyaridhia na huyakubali.
2 – Mja hufanya matendo kimazoea na katika hali ya kughafilika, lakini ananuia kwayo utiifu na kujikurubisha kwa Allaah. Viungo vyake vinashughulika na utiifu lakini moyo wake umesahau kumtaja Allaah. Hivyo ndivyo ilivyo kwa matendo yake yote. Basi yanapoinuliwa matendo ya huyu kwa Allaah (´Azza wa Jall) hayasimami mbele Yake wala haangalii kwake, bali huwekwa mahala pa kuwekwa majalada ya matendo hadi yatawasilishwa kwake siku ya Qiyaamah. Hapo yatatofautishwa; Atamlipa kwa yale yaliyokuwa kwa ajili Yake na kumrudishia yale ambayo hayakuwa kwa ajili ya uso Wake. Kupewa thawabu juu ya matendo hayo ni kumlipa mja kupitia kiumbe miongoni mwa viumbe Wake, kama majumba, chakula, vinywaji na wake wa Peponi. Lakini thawabu ya yule wa mwanzo ni ridhaa juu ya matendo yenyewe, radhi ya Allaah juu ya mja huyo, kumkaribia kwake na kuinuliwa daraja yake na cheo chake. Huyu hulipwa thawabu bila hesabu. Kwa hiyo kuna tofauti kati ya mtu wa kwanza na mtu wa pili.
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 48-49
Imechapishwa: 06/08/2025
https://firqatunnajia.com/28-matendo-mawili-yanayokubaliwa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket