28. Hatuna kasumba; Qur-aan, Sunnah na Salaf

26 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia:

“Alikuja bwana mmoja akasema: “Ee Ibn ´Abbaas! Mimi naona ndani ya Qur-aan kuna mambo yanayogongana, na yanatia dukuduku moyoni mwangu.” Ibn ´Abbaas akasema: “Ukadhibishaji?” Akasema: “Sio ukadhibishaji, lakini tofauti.” Akasema: “Nieleze yale yanayoutia dukuduku moyo wako.” Akasema: “Sikia namna ambavyo Allaah anasema:

أَأَنتُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَمِ السَّمَاءُۚ بَنَاهَا رَفَعَ سَمْكَهَا فَسَوَّاهَا وَأَغْطَشَ لَيْلَهَا وَأَخْرَجَ ضُحَاهَا وَالْأَرْضَ بَعْدَ ذَٰلِكَ دَحَاهَا

”Je, uumbwaji wenu ndio vigumu zaidi au mbingu Aliyoijenga? Amenyanyua kimo chake akazisawazisha; na akatia kiza usiku wake na akatokezesha mwanga wa mchana wake. Na ardhi baada ya hayo akaitandaza.”

Hapa ametaja kuwa ameumba mbingu kabla ya ardhi. Ilihali katika Aayah nyingine anasema:

وَجَعَلَ فِيهَا رَوَاسِيَ مِن فَوْقِهَا وَبَارَكَ فِيهَا وَقَدَّرَ فِيهَا أَقْوَاتَهَا فِي أَرْبَعَةِ أَيَّامٍ سَوَاءً لِّلسَّائِلِينَ ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ وَهِيَ دُخَانٌ

”Akaweka humo milima iliyosimama imara juu yake, na akabariki humo kwa kheri zisizokatika, na akakadiria humo chakula chake kwenye siku nne – ni idadi madhubuti kwa waulizaji. Kisha Akalingana juu ya mbingu, nazo ni moshi.”[1]

Hapa anataja kuwa ameziumba ardhi kabla ya mbingu.” Ibn ´Abbaas akasema: “Kuhusu maneno Yake:

أَأَنتُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَمِ السَّمَاءُۚ بَنَاهَا رَفَعَ سَمْكَهَا فَسَوَّاهَا وَأَغْطَشَ لَيْلَهَا وَأَخْرَجَ ضُحَاهَا وَالْأَرْضَ بَعْدَ ذَٰلِكَ دَحَاهَا

”Je, uumbwaji wenu ndio vigumu zaidi au mbingu Aliyoijenga? Amenyanyua kimo chake akazisawazisha; na akatia kiza usiku wake na akatokezesha mwanga wa mchana wake. Na ardhi baada ya hayo akaitandaza.”,

maana yake ni kwamba ameziumba ardhi ndani ya siku mbili kabla ya mbingu. Kisha baada ya hapo akalingana juu ya mbingu na akaziumba ndani ya siku mbili zingine. Halafu akashuka ardhini na akaitandaza,  maana yake ni kuleta maji na malisho yake.”

Ameipokea al-Bukhaariy[2].

[1] 41:10-11

[2] Amefanya hivo hali ya kuwa na cheni ya wapokezi pungufu na vilevile iliyoungana. Vivyo hivyo ameipokea al-Bayhaqiy kwa cheni ya wapokezi ilioungana katika ”al-Asmaa’ was-Swifaat”, uk. 379, na Abush-Shaykh katika ”al-´Adhwamah” (1/100).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 94
  • Imechapishwa: 24/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy