113 – Abul-Hasan Muhammad bin Ahmad bin Muhammad bin Ahmad bin Rizq al-Bazzaaz na Abul-Husayn ´Aliy bin Muhammad bin ´Abdillaah al-Mu-addil wametukhabarisha: Abu ´Aliy Ismaa´iyl bin Muhammad bin Ismaa´iyl as-Swaffaar ametuzindua: Abu Yahyaa Zakariyyaa bin Yahyaa bin Asad al-Marwaziy ametuhadithia… (ح) al-Qaadhwiy Abu Bakr Ahmad bin al-Hasan bin Ahmad al-Harashiy ametuzindua: Abul-´Abbaas Muhammad bin Ya´quub al-Aswamm ametuhadithia: Zakariyyaa bin Yahyaa al-Marwaziy ametuhadithia: Ma´ruuf al-Karkhiy ametuhadithia: Bakr bin Khunays amesema:

”Hakika Motoni kuna bonde ambalo Jahannam inaomba ulinzi dhidi yake kila siku mara saba. Katika bonde hilo kuna shimo ambalo bonde lenyewe na Jahannam vinaomba ulinzi dhidi yake kila siku mara saba. Ndani ya shimo hilo kuna nyoka ambayo shimo lenyewe, bonde na Jahannam vinaomba ulinzi dhidi yake kila siku mara saba. Wa mwanzo watakaoingia ndani yake ni watenda maasi wenye kuisoma Qur-aan, ambapo waseme: ”Ee Mola! Tumeanza kuingia sisi kabla ya wenye kuabudia masanamu?” Waambiwe: ”Ambaye anajua si kama ambaye hajui.”

114 – ´Abdur-Rahmaan bin Ahmad al-Qazwiyniy ametuhadithia: ´Aliy bin Ibraahiym bin Salamah al-Qattwaan ametuzindua: Abu Haatim ar-Raaziy ametuhadithia: Hudbah ametuhadithia: Sallaam – yaani Ibn Abiy Mutwiy´ – ametuhadithia: Nimemsikia Ayyuub as-Sakhtiyaaniy akisema:

”Hakuna mtenda dhambi muovu zaidi kama msomaji Qur-aan muovu.”

115 – Abu Haatim amesema: Hudbah ametukhabarisha: Hazm – yaani al-Qutw´ayiy – ametukhabarisha: Nimemsikia Maalik bin Diynaar akisema:

”Hakika mimi nakhofia zaidi juu ya msomaji Qur-aan mtenda dhambi kuliko ninavyokhofia juu ya mtenda dhambi anayefanya waziwazi maovu yake, kwa sababu huyu yu mbali zaidi na kujighuri.”

116 – Abul-Qaasim Bakraan bin at-Twayyib bin al-Hasan as-Saqatwiy amenikhabarisha huko Jarjaraayaa: Muhammad bin Ahmad bin Muhammad bin Ya´quub al-Mufiyd ametuhadithia: Ahmad bin al-Hasan bin ´Abdil-Jabbaar na Ahmad bin ´Aliy bin al-Muthannaa wametuhadithia: ´Abdus-Swamad bin Yaziyd ametuhadithia: Nimemsikia al-Fudhwayl akisema:

”Hakika mambo yalivyo ni kwamba Qur-aan imeteremshwa ili ifanyiwe kazi kwa matendo ambapo watu wakafanya usomaji wake kuwa ni kazi.” Ni vipi inafanyiwa kazi” Akasema: ”Kwa kuhalalisha ya halali yake, kuharamisha ya haramu yake, kutii amri zake na kukomeka na makatazo yake.”

117 – Abul-Hasan Muhammad bin ´Umar bin ´Iysaa bin Yahyaa al-Baladiy amenikhabarisha: Muhammad bin al-´Abbaas bin al-Fadhwl bin Yuunus al-Khayyaatw amenikhabarisha huko Mosul: Muhammad bin Ahmad bin Abiyl-Muthannaa amenikhabarisha: Qabiyswah bin ´Uqbah amenikhabarisha, kutoka kwa Sufyaan ath-Thawriy, kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa Abu Raziyn, amesema kuhusu maneno Yake (Ta´ala):

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلَاوَتِهِ

“Wale Tuliowapa Kitabu wanakisoma kwa haki ipasavyo kusomwa kwake.”[1]

”Wanaifuata vile inavyopasa kufuatwa. Wanaifanyia kazi yale yanayopasa kufanyiwa kazi.”

118 – al-Qaadhwiy Abu Muhammad Yuusuf bin Rabaah bin ´Aliy al-Baswriy amenikhabarisha: Abu ´Abdillaah Muhammad bin al-Muhsin bin al-Husayn al-Azdiy ametuhadithia huko Misri: al-´Abbaas bin Ahmad al-Khawaatimiy ametukhabarisha huko Twarsus: al-´Abbaas bin al-Fadhwl al-Arsuufiy ametukhabarisha: Ahmad bin ´Abdil-´Aziyz ametukhabarisha: Naswr bin ´Iysaa ametukhabarisha: Maalik bin Anas ametukhabarisha, kutoka kwa Naafiy´, kutoka kwa Ibn ´Umar, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema kuhusu maneno Yake (Ta´ala):

يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلَاوَتِهِ

“… wanakisoma kwa haki ipasavyo kusomwa kwake.”

”Wanaifuata vile inavyopasa kufuatwa.”[2]

[1] 2:121

[2] Cheni ya wapokezi ni dhaifu. adh-Dhahabiy amemtuhumu al-´Abbaas bin al-Fadhwl al-Arsuufiy kutunga Hadiyth. Msimuliaji wa al-Khawaatiymiy hatambuliki. Vivyo hivyo kuhusu Ahmad bin ´Abdil-´Aziyz na Naswr bin ´Iysaa. adh-Dhahabiy na Ibn Hajar wote wawili wameitaja Hadiyth hii na wakasema:

”al-Khatwiyb amesema ”katika mlolongo wa wapokezi wake kuna watu wengi wasiotambulika”.”

al-Khatwiyb ameyasema haya katika “ar-Ruwaat ´an Maalik”. as-Suyuutwiy ameinasibisha Hadiyth hii katika kitabu hicho na akasema:

”Cheni ya wapokezi ina wasimuliaji wasiotambulika.” (ad-Durr al-Manthuur (1/111))

Hadiyth ameipokea pia Ibn Jariyr na al-Haakim (2/266) kwa njia ya maneno ya Ibn ´Abbaas, jambo ambalo ndio la sawa.

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 75-77
  • Imechapishwa: 21/05/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy