93 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema katika Rukuu´ na Sujuud yake:

سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي

“Kutakasika ni Kwako, ee Allaah Mola wetu, na himdi zote ni Zako. Ee Allaah! Nisamehe.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

MAELEZO

Hadiyth hii inafahamisha kuwa ni jambo limewekwa katika Shari´ah kusema:

سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي

“Kutakasika ni Kwako, ee Allaah Mola wetu, na himdi zote ni Zako. Ee Allaah! Nisamehe.”

katika Sujuud na Rukuu´. Lakini kusema hivo ni baada ya yeye kusema katika Rukuu´:

سُبْحانَ رَبِّيَ الْعَظِيمِ

“Ametakasika, Mola wangu, Aliye mtukufu.”

Na baada ya kusema katika Sujuud:

سُبْحَانَ رَبِّيَ الأَعْلَى

“Ametakasika, Mola wangu, Aliye juu.”

Jengine ni kwamba Rukuu´, ingawa si mahali pa kuomba du´aa, kama ilivyokuja katika Hadiyth:

“Kuhusu Rukuu´ mtukuzeni ndani yake Mola.”

Hata hivyo du´aa hii ni ndogo inayofuata baada ya Dhikr na kusifiwa kwa Allaah. Kwa hivyo tumewekewa nayo katika Shari´ah katika Rukuu´ na Sujuud.

[1] al-Bukhaariy (794) na Muslim (484).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 96-97
  • Imechapishwa: 29/10/2025