27. Mwenye kujitahidi kuitafuta dunia ataidhuru Aakhirah

161 – Hadiyyah bin ´Abdil-Wahhaab ametukhabarisha: al-Fadhwl bin Muusa ametukhabarisha: Muhammad bin ´Amr ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kujitahidi kuitafuta dunia atairudhuru Aakhirah, ma mwenye kujitahidi kuitafuta Aakhirah atairudhuru dunia.” Nilimsikia akisema: “Hakikisha kwamba unadhuru kitu kitachotokomea kwa ajili ya kitu kitachodumu.”

162 – Abu Bakr bin Abiy Shaybah ametukhabarisha: Khaalid bin Makhlad ametukhabarisha: Sulaymaan bin Bilaal ametukhabarisha, kutoka kwa ´Amr bin Abiy ´Amr, kutoka kwa al-Muttwalib bin Hantwab, kutoka kwa Abu Muusa al-Ash´ariy, ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kupenda ulimwengu ataidhuru Aakhirah, na mwenye kuipenda Aakhirah ataidhuru dunia yake. Basi pendeleeni kitachotokomea kwa ajili ya kitachodumu.”[1]

[1] Ahmad (19198) na al-Haakim (4/354). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “as-Swahiyhah” (3287).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 39
  • Imechapishwa: 06/07/2025