Muqtadha ya kushuhudia ya kwamba “Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah”. Ni kule kuacha kuabudu mwengine asiyekuwa Allaah katika  vinavyoabudiwa vyote. Hayo ndio yanayofahamishwa na makanusho pale tunaposema “Hapana mungu wa haki”. Sambamba na hilo mtu akamwabudu Allaah, hali ya kuwa pekee yake hana mshirika. Hayo ndio yanayofahamishwa na uthibitishaji pale tunaposema “Isipokuwa Allaah”. Wengi wanaolitamka wanakwenda kinyume na muqtadha yake na hivyo utawaona wanathibitisha uungu wa viumbe vile vilivyokanushwa, makaburi, makuba, waungu wa batili, miti na mawe. Watu hawa wameitakidi kuwa eti Tawhiyd ni Bid´ah, wakamkaripia yule anayewalingania kwayo na wakamkejeli yule anayemtakasia ´ibaadah Allaah.

2- Muqtadha ya kushuhudia ya kwamba “Muhammad ni Mtume wa Allaah”. Ni kule kumtii, kumsadikisha, kuacha yale aliyokataza, kukomeka juu ya kutendea kazi Sunnah, kujiepusha  na vyenginevyo katika Bid´ah na mambo mepyamepya yaliyozuliwa na kutanguliza maneno yake mbele ya maneno ya mwengine yeyote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 51
  • Imechapishwa: 20/02/2020