Kuhusu kuweka mazulia kwenye misikiti, hapana shaka kwamba kitendo hicho kinamsh kunamshughulisha mwenye kuswali. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:
”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwenye vazi lenye mifumo na akatazama mifumo yake. Alipomaliza akasema: “Ipelekeni kanzu hii kwa Abu Jahm na mniletee nguo nyingine ya Abu Jahm isiyo na michoro. Inanishughulisha kutokamana na swalah yangu.”[1]
Imekuja katika upokezi mwingine:
“Kwani nimetazama mifumo yake katika swalah na imekaribia kunitia katika mtihani.”
Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:
”´Aaishah alitundika pazia la kitambaa kilichokuwa na michoro upande wa nyumba yake, ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ondoa pazia hili kwangu, kwani picha zake zinaendelea kujitokeza mbele yangu wakati wa swalah yangu.”[2]
´Uqbah bin ´Aamir (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:
”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipewa zawadi ya vazi la hariri. Akalivaa na kuswali nalo. Alipomaliza, alilivua kwa nguvu kama mtu aliyelichukia, na akasema: “Hili halitakikani kwa wanaomcha Allaah.”[3]
as-Swan´aaniy amesema kuhusiana na Hadiyth ya ´Aaishah ya kanzu yenye michoro:
”Katika Hadiyth hii kuna dalili ya kwamba kila kinachoshughulisha mswaliji, kama vile michoro na mfano wake, kwamba kinachukiza. Hadiyth inathibitisha pia kuchukua kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hatua ya haraka kuhifadhi swalah kutokana na vitu vyovyote vinavyoweza kushughulisha na kuondoa chochote kinachoweza kuvuruga kumshughulisha mtu na kuizingatia.”[4]
at-Twibiy amesema:
”Hadiyth hii inaashiria kuwa picha na vitu vyenye sura dhahiri vina athari katika nyoyo safi na roho zilizo zenye takasika, sembuse vyengine vyote vilivyo chini ya kiwango hicho. Jengine ni kwamba inachukiza kuswali kwenye mikeka na mazulia yenye michoro na misikiti iliyopambwa na mfano wake.”
[1] al-Bukhaariy (752) na Muslim (556).
[2] al-Bukhaariy (374).
[3] al-Bukhaariy (5801) na Muslim (2075).
[4] Subul-us-Salaam.
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 31-32
- Imechapishwa: 23/06/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket