11 – Kukataa kuolewa kwa hoja ya kusoma

Miongoni mwa makosa yanayopingana na Shari´ah ni baadhi ya wasichana kukataa kuolewa kwa kisingizio cha kusoma. Ndoa haipingani na kusoma wala kufundisha. Bali tunaona kuwa wanafunzi wa kike ambao tayari wamekwishaolewa fikira yao inakuwa yenye kutulia na wanapata faida zaidi kuliko wale wanafunzi wa kike ambao hawajaolewa. Mambo ni vivyo hivyo inapokuja kwa wanaume. Kwa hiyo usikatae ndoa anapokujilia mtu ambaye anakufaa, kwa sababu pengine vijana wakajiweka mbali na wewe baada ya kumaliza masomo yako kutokana na uzee kisha ukajuta na hali ya kuwa majuto ni mjukuu.

  • Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 29
  • Imechapishwa: 27/02/2026