Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) amebainsha ya kwamba ameikamilisha dini na akawakamilishia neema Yake kupitia yeye (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Aidha akamwamrisha afikishe ujumbe Wake. Kama alivyosema (Ta’ala):
الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا
”Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema Yangu na nimekuridhieni kwenu Uislamu uwe ndio dini yenu.”[1]
يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ
“Ee Mtume! Fikisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako. Na usipofanya, basi utakuwa hukufikisha ujumbe Wake. Na Allaah atakuhifadhi kutokamana na watu.”[2]
Kwa msemo mwingine ni “haiwezekani kabisa kwamba akaacha jambo ambalo ndio lengo kuu la kuwaumba viumbe, Mitume wakatumilizwa kwalo, Vitabu vikateremshwa kwa jambo hilo, Qiblah kikawekwa kwa jambo hilo na msingi ukajengwa juu yake, nalo ni kumwamini Yeye na kumtambua, majina Yake, Sifa Zake, vitendo Vyake ambapo haki ikachanganyikana na batili na akanyamazia haki katika suala hilo. Bali amezungumza kwa yale ambayo udhahiri wake ni batili na yasifahamike kwa udhahiri wake. Itakuweje kwa ambaye ndiye Mtume bora kabisa na Kitabu kitukufu zaidi watashindwa kufafanua somo hilo kwa njia ambayo ni kamili, bainifu na iliyo wazi zaidi? Suala hilo ni muhimu sana ikizingatiwa kwamba watu wako katika hitaji kubwa sana la kumjua Yeye. Isitoshe ujuzi huo ndio ujuzi bora na tukufu zaidi ambao wanadamu wanaweza kupata. Haiwezekani kabisa kwamba Mtume bora kabisa (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliwafundisha ummah wake adabu inayohusiana na kukojoa, kujamiiana, kula na kunywa na sambamba na hayo akapuuza kuwafundisha nini wanachotakiwa kusema na kuamini juu ya Mola na Mwabudiwa wao. Kwani kumjua Yeye ndio utambuzi wa hali ya juu, kuwasili Kwake ndio lengo tukufu zaidi na kumuabudu Yeye pekee ndio njia iliyo karibu zaidi. Je, hivi yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) angezungumza kwa njia ambayo udhahiri wake ni batili na ukafiri na hivyo akawaelekeza kwenye tafsiri zenye kuchukiza na mafumbo yenye kukemewa na hatimaye akawaacha waitambue haki kutokana na vile itavyohukumu akili na maoni yao wenyewe? Si yeye ndiye amesema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):
“Nimekuacheni katika njia nyeupe kabisa; usiku wake ni kama usiku wake. Hatopotea nayo baada yangu isipokuwa mwangamivu.”[3]
Yeye ndiye amesema:
“Allaah hakutuma Mtume yeyote isipokuwa ilikuwa ni wajibu kwake kuwaelekeza Ummah wake katika yale yenye kheri anayoyajua kwao na kuwakataza yale yenye shari anayoyajua kwao.”[4]
Abu Dharr (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakufa na kumwacha ndege anayepiga kwa mbawa zake mbinguni isipokuwa ametufunza kitu juu yake.”[5]
´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alituhadithia kila kitu kuanza kwa uumbaji mpaka pale ambapo watu wa Peponi watakapoingia kwenye makazi yao na watu wa Motoni watakapoingia kwenye makazi yao. Aliyahifadhi hayo mwenye kuyahifadhi na aliyasahau mwenye kuyasahau.”[6]
Vipi mtu anayemuogopa Allaah, Mtume Wake na dini Yake, anaweza kuona kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliacha kubainisha jambo hili kubwa na asizungumze yaliyo ya sawa, bali badala yake akazungumza yale ambayo udhahiri wake ni kinyume na usawa? Bali imani ya mtu haikamiliki mpaka aamini kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ameibainisha kikamilifu na kwa uwazi kabisa na hakuacha nafasi kwa yeyote kueleza au kufasiri. Isioshe haiwezekani kabisa kwamba aliye bora zaidi, mjuzi zaidi, aliyetangulia katika kila sifa tukufu, mwongozo na ujuzi kwamba alipuuza katika suala hili, kwa namna ya kwamba akakabiliana nalo kwa kuzembea, au akalichupia mipaka, na hivyo akavuka mipaka yake”[7].
[1] 5:3
[2] 5:67
[3] Ahmad (4/126), Ibn Maajah (43) na al-Haakim (1/95).
[4] Muslim (1844).
[5] Ahmad (5/153), al-Bazzaar (3897) na at-Twabaraaniy (1647).
[6] al-Bukhaariy (3192) na Muslim (2891).
[7] as-Swawaa´iq al-Mursalah (1/157-160) ya Ibn-ul-Qayyim. Tazama “al-Hamawiyyah”, uk. 7, ya Ibn Taymiyyah.
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 46-48
- Imechapishwa: 01/12/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 46-48
Imechapishwa: 01/12/2025
https://firqatunnajia.com/27-iisingeliwezekana-kuacha-kubainisha/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket