27. Hivi ndivo alivokuwa akifanya Mtume wakati inaponyesha mvua

25 –  Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiondosha nguo yake kutoka mabegani ili maji yampate, na akisema: ”Ndio punde imetoka kwa Mola wake.”[1]

Ameipokea Muslim.

[1] Tamko lake ni ifuatavyo kama alivosema Anas:

”Tulipatwa na mvua wakati tulipokuwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akavua nguo yake, ili maji ya mvua yampate. Tukasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Ni kwa nini umefanya hivi?” Akasema: ”Kwa sababu ndio punde imetoka kwa Mola wake.”

Hivo pia ndivo ameipokea Abu Daawuud na Ahmad (3/133) na (3/267). Tamko lilioko kwenye kitabu ni la Haafidhw Abul-Qaasim al-Baghawiy. Mtunzi ameipokea Hadiyth kutoka kwake. Hadiyth ipo katika “as-Sunnah” (823) ya Ibn Abiy ´Aaswim na katika “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”, uk. 25 ya ad-Daarimiy.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 93-4
  • Imechapishwa: 24/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy