27. Hadiyth “Ni nchi gani zinazopendwa zaidi na Allaah… “

325 – Jubayr bin Mutw´im (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

أنَّ رجُلاً قال: يا رسولَ الله! أيُّ البُلدان أحبُّ إلى الله، وأي البُلدان أبغضُ إلى الله؟ قال: “لا أدري، حتى أسألَ جبريل عليه السلام ، فأتاه جبريل، فأخبرَه

.”أنَّ أحسنَ البِقاع إلى الله المساجدُ، وأبغضَ البِقاع إلى الله الأسواقُ”

“Bwana mmoja alisema: “Ee Mtume wa Allaah! Ni nchi gani zinazopendwa zaidi na Allaah na ni nchi gani zinazochukiwa zaidi na Allaah?” Akasema: “Sijui mpaka nimuulize Jibriyl (´alayhis-Salaam).” Ndipo akamjia Jibriyl na kumweleza: “Maeneo yanayopendwa zaidi na Allaah ni misikiti na maeneo yanayochukiwa zaidi na Allaah ni masoko.”[1]

Ameipokea Ahmad, al-Bazzaar na tamko ni lake, Abu Ya´laa na al-Haakim ambaye amesema:

“Ni yenye cheni ya wapokezi Swahiyh.”

[1] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/248-249)
  • Imechapishwa: 02/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy