92 – Mutwarrif bin ´Abdillaah bin ash-Shukhayr (Radhiya Allaahu ´anh) amepokea kuwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amemsimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema katika Rukuu´ na Sujuud yake:

سُبُّوُحٌ، قُدُّوسٌ، رَبُّ المَلاَئِكَةِ وَالرُّوحِ

“Mwingi wa kutakaswa, mtakatifu, Mola wa Malaika na roho [Jibriyl].”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Maana yake ni, ee Ambaye umesafika kutokana na mapungufu na ee Ambaye umetakasika kutokana na yale yasiyokustahiki, utakasifu ni Wako.

[1] Muslim (487).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 96
  • Imechapishwa: 29/10/2025