Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
Amesema (Ta´ala) amesema:
قَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا وَتَشْتَكِي إِلَى اللَّـهِ وَاللَّـهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَا ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ
”Hakika Allaah amekwishasikia kauli ya yule mwanamke anayejadiliana nawe kuhusu mumewe na anamshitakia Allaah; na Allaah anayasikia majibizano yenu – hakika Allaah ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (58:01)
لَّقَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ فَقِيرٌ وَنَحْنُ أَغْنِيَاءُ
”Kwa hakika Allaah ameisikia kauli ya wale [mayahudi] ambao wamesema: “Hakika Allaah ni fakiri na sisi ni matajiri”.” (03:181)
أَمْ يَحْسَبُونَ أَنَّا لَا نَسْمَعُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُم ۚ بَلَىٰ وَرُسُلُنَا لَدَيْهِمْ يَكْتُبُونَ
”Au wanadhania kwamba Sisi Hatusikii siri zao na minong’ono yao? Sivyo! [Tunasikia!] na Wajumbe wetu wako kwao wanaandika.” (43:80)
إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَىٰ
”Hakika Mimi niko pamoja nanyi, nasikia na naona.” (20:46)
أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ اللَّـهَ يَرَىٰ
”Je, hajui kwamba Allaah anaona?” (96:14)
وَتَوَكَّلْ عَلَى الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ الَّذِي يَرَاكَ حِينَ تَقُومُ
”Mtegemee Mwenye nguvu mshindi, Mwenye kurehemu, ambaye anakuona wakati unaposimama.” (26:217-218)
وَقُلِ اعْمَلُوا فَسَيَرَى اللَّـهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ وَالْمُؤْمِنُونَ
”Na sema [uwaambie]: “Fanyeni matendo! Allaah atayaona matendo yenu na Mtume Wake na waumini.” (09:105)
وَهُوَ شَدِيدُ الْمِحَالِ
”Naye ni mkali wa kusibu misiba na maangamizi.” (13:13)
وَمَكَرُوا وَمَكَرَ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ
”Wakapanga njama, lakini Allaah akapanga [kuwalipiza] njama – na Allaah ni mbora wa kurudisha njama za wenye kupanga njama.” (03:54)
وَمَكَرُوا مَكْرًا وَمَكَرْنَا مَكْرًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ
”Wakapanga njama – Nasi tukapanga mipango ya kuvurumisha njama [zao kwa kuwaadhibu], nao huku hawatambui.” (27:50)
إِنَّهُمْ يَكِيدُونَ كَيْدًاوَأَكِيدُ كَيْدًا
”Hakika wao wanapanga njama, Nami napanga mipango [ya kuvunja na kupindua njama zao].” (86:15-16)
إِن تُبْدُوا خَيْرًا أَوْ تُخْفُوهُ أَوْ تَعْفُوا عَن سُوءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَفُوًّا قَدِيرًا
”Mkidhihirisha kheri au mkiificha au mkisamehe uovu; basi hakika Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Muweza.” (04:149)
وَلْيَعْفُوا وَلْيَصْفَحُوا ۗ أَلَا تُحِبُّونَ أَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
”Wasamehe na waachilie mbali. Je, [nyinyi] hampendi Allaah akusameheni? Na Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (24:22)
وَلِلَّـهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ
”Na hali utukufu ni wa Allaah na wa Mtume Wake na wa waumini.” (63:08)
Ameeleza (Tabaarak wa Ta´ala) ya kwamba Ibliys amesema:
فَبِعِزَّتِكَ لَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ
“Naapa kwa Utukufu Wako, bila shaka nitawapotosha wote.” (38:82)
Allaah (Subhaanah) Amesema:
تَبَارَكَ اسْمُ رَبِّكَ ذِي الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ
”Limebarikika jina la Mola wako, Mwenye utukufu na ukarimu!” (55:78)
فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ ۚ هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا
”Basi mwabudu Yeye tu na dumisha subira katika ‘ibaadah Yake. Je, unamjua [mwengine] mwenye jina Lake? (19:65)
وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
“… na wala hana yeyote anayefanana [wala kulingana] Naye.” (112:04)
MAELEZO
Allaah anasifika tu kufanya njama pale tu inapohusiana na kulipiza njama:

”Wakapanga njama, lakini Allaah akapanga [kuwalipiza] njama – na Allaah ni mbora wa kurudisha njama za wenye kupanga njama.”

”Hakika wao wanapanga njama Nami napanga mipango [ya kuvunja na kupindua njama zao].”
Ni njama zinazolingana na Allaah. Hafanani na viumbe Wake katika kupanga Kwake njama na vitimbi Vyake.
Vivyo hivyo inahusiana na usikizi. Amesema (Ta´ala):

”Hakika Allaah amekwishasikia kauli ya yule mwanamke anayejadiliana nawe kuhusu mumewe na anamshitakia Allaah; na Allaah anayasikia majibizano yenu – hakika Allaah ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”
إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
“Hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi.”
إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ
“Hakika Allaah ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”
Kuna Aayah nyenginezo nyingi zenye kuthibitisha usikizi, ujuzi na uoni.
Vilevile kuna Aayah nyingi zenye kuthibitisha kupenda. Zote hizo ni haki na ni wajibu kumthibitishia nazo Allaah kwa njia yenye kulingana Naye:
هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا
“Je, unamjua [mwengine] mwenye jina kama Lake?”
وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
“… na wala hana yeyote anayefanana [wala kulingana] Naye.”
فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ
”Basi msipigie mifano Allaah!”
Zote hizi ni [sifa za] haki na ni wajibu kumthibitishia nazo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa njia inayolingana na Allaah pasi na upotoshaji, ukanushaji na kuzipindisha maana. Ana usikizi na sio kama usikizi wetu, ana uoni na sio kama uoni wetu, macho sio kama macho yetu, mkono sio kama mkono wetu, nguvu na sio kama nguvu zetu. Hali kadhalika inahusiana na sifa zingine zote. Anasema (Subhaanah):
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (42:11)
Sifa za Allaah ni haki na ni zenye kulingana na Yeye. Sifa Zake hazifananishwi na viumbe Vyake (Jalla wa ´Alaa). Ni wajibu kumthibitishia nazo Allaah kwa njia yenye kulingana Naye bila ya kupotosha, kukanusha, kuzifanyia namna wala kuzifananisha. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaona kuwa zote zinatakiwa kufahamika kwa njia moja na kwa mtindo mmoja. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wale wenye kuwafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 37-38
- Imechapishwa: 21/10/2024

Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 37-38
Imechapishwa: 21/10/2024
https://firqatunnajia.com/27-dalili-ya-usikizi-uoni-ujuzi-na-njama-za-allaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)