Swali 27: Ni vipi muislamu ataswali ndani ya ndege? Je, ni bora kwake kuswali ndani ya ndege mwanzoni mwa wakati au kusubiri mpaka atakapofika katika uwanja wa ndege ikiwa atafika mwishoni mwa wakati?
Jibu: Ni lazima kwa muislamu ndani ya ndege utapofika wakati wa swalah basi aiswali kwa kiasi cha uwezo wake. Akiweza kuswali kwa kusimama na akarukuu na kusujudu basi atafanya hivo. Asipoweza basi ataswali kwa kuketi na ataashiria Rukuu´ na Sujuud. Akipata maeneo ndani ya ndege ambapo anaweza kusimama, kusujudu ardhini badala ya kuashiria, basi kutamlazimu kufanya hivo. Allaah (Subhaanah):
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia ´Imraan bin Huswayn (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kipindi ambapo alikuwa mgonjwa:
”Swali kwa kusimama. Usipoweza, kwa kukaa. Usipoweza, lalia bavu.”
Ameipokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake.
an-Nasaa´iy pia ameipokea kwa cheni ya wapokezi Swahiyh na akaongeza:
“Asipoweza, basi kwa kuegemea.”
Bora kwake ni yeye aswali mwanzoni mwa wakati. Hapana neno akichelewesha mpaka mwishoni mwa wakati ili aiswali juu ya ardhi kutokana na kuenea kwa dalili. Gari, treni na meli ina hukumu moja kama ya ndege.
[1] 64:16
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 29-30
- Imechapishwa: 21/08/2022
Swali 27: Ni vipi muislamu ataswali ndani ya ndege? Je, ni bora kwake kuswali ndani ya ndege mwanzoni mwa wakati au kusubiri mpaka atakapofika katika uwanja wa ndege ikiwa atafika mwishoni mwa wakati?
Jibu: Ni lazima kwa muislamu ndani ya ndege utapofika wakati wa swalah basi aiswali kwa kiasi cha uwezo wake. Akiweza kuswali kwa kusimama na akarukuu na kusujudu basi atafanya hivo. Asipoweza basi ataswali kwa kuketi na ataashiria Rukuu´ na Sujuud. Akipata maeneo ndani ya ndege ambapo anaweza kusimama, kusujudu ardhini badala ya kuashiria, basi kutamlazimu kufanya hivo. Allaah (Subhaanah):
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia ´Imraan bin Huswayn (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kipindi ambapo alikuwa mgonjwa:
”Swali kwa kusimama. Usipoweza, kwa kukaa. Usipoweza, lalia bavu.”
Ameipokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake.
an-Nasaa´iy pia ameipokea kwa cheni ya wapokezi Swahiyh na akaongeza:
“Asipoweza, basi kwa kuegemea.”
Bora kwake ni yeye aswali mwanzoni mwa wakati. Hapana neno akichelewesha mpaka mwishoni mwa wakati ili aiswali juu ya ardhi kutokana na kuenea kwa dalili. Gari, treni na meli ina hukumu moja kama ya ndege.
[1] 64:16
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 29-30
Imechapishwa: 21/08/2022
https://firqatunnajia.com/27-bora-kuswali-ndani-ya-ndege-mwanzoni-mwa-wakati-au-kusubiri-ideme/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)