27. Bid´ah zinazofanyika wakati wa Sa´y kati ya Swafaa na Marwah

63- Kutawadha kwa ajili ya kutembea baina ya Swafaa na Marwah kwa madai kwamba yule mwenye kufanya hivo kwa kila hatua anayopiga analipwa daraja elfu sabini.

64- Kupanda juu Swafaa mpaka mtu aguse ukuta.

65- Kuomba du´aa wakati mtu anaposhuka Swafaa:

اللهم استعملني بسنة نبيك وتوفني على ملته وأعذني من مضلات الفتن برحمتك يا أرحم الراحمين

“Ee Allaah! Nijaalie niweze kufuata Sunnah za Mtume wako na unifishe juu ya dini yake na unilinde kutokamana na fitina zinazopotosha. Kwa huruma Wako, ee Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.”

66- Kusema wakati wa Sa´y:

رب اغفر وارحم وتجاوز عما تعلم إنك أنت الأغر الأكرم اللهم اجعله حجا مبرورا أو عمرة مبرورة وذنبا مغفورا الله أكبر ثلاثا

“Mola nisamehe, unirehemu na unifutie yale unayoyajua. Kwani Wewe ni mtukufu, mwenye huruma. Ee Allaah! Ifanye kuwa ni hajj yenye kukubaliwa au ´Umrah yenye kukubaliwa na dhambi yenye kusamehewa. Allaahu Akbar! Allaahu Akbar! Allaahu Akbar!”[1]

67- Kufanya Sa´y mizunguko kumi na nne na mzunguko wa mwiso mtu anamalizia Swafaa.

68- Kuirudia Sa´y mara kwa mara katika hajj au ´umrah.

69- Kuswali Rak´ah mbili baada ya kumaliza Sa´y.

70- Kuendelea kufanya Sa´y baina ya Swafaa na Marwah baada ya kukimiwa swalah mpaka swalah ya mkusanyiko inawapita.

71- Kulazimiana na du´aa maalum pindi mtu anapofika Minaa. Kama mfano ile iliyotajwa katika “al-Ihyaa´”:

اللهم هذه منى فامنن علي بما مننت به على أوليائك وأهل طاعتك

“Ee Allaah! Hii ni Minaa. Neemesha juu yangu kwa yale Uliyoneemesha mawalii Wako na wale wenye kukutii… “

Pindi mtu anapotoka Minaa, imekuja kwamba mtu aseme:

اللهم اجعلها خير غدوة غدوتها قط

“Ee Allaah! Ifanye kuwa ni matokeo mazuri ambayo nimewahi kutokea… “

[1] Hata hivyo imesihi kutoka kwa Maswahabah Ibn Mas´uud na Ibn ´Umar kwamba wamesema:

رب اغفر وارحم وأنت الأعز الأكرم كما تقدم

“Mola! Nisamehe na unirehemu. Hakika Wewe ni Mwenye nguvu kabisa, mkarimu.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah, uk. 50
  • Imechapishwa: 21/07/2018