Hivyo ni juu ya muislamu ajihadhari na kughafilika na kumtaja Allaah (´Azza wa Jall), asije akachukua sehemu ya mwanzo ya Hadiyth na akaacha sehemu yake ya mwisho. Na ni juu yake kuzijaza nyakati hizi tukufu kwa utiifu na kutenda mema wala asizipoteze kwa upuuzi na michezo, kama wanavyofanya wengi wa watu katika zama hizi ambapo wanakesha, kukosa swalah za faradhi ndani ya wakati wake, kupoteza muda na kutumia neema za Allaah kwa kumuasi na kushikamana na vyombo vya upuuzi na miziki.

Fahamu kwamba haijuzu kufunga siku za Tashriyq. Basi atakayekuwa na ada ya kufunga siku ya alkhamisi asifunge ikiwa itakutana na siku hizo. Vilevile inahusu masiku meupe asifunge tarehe 13. Isipokuwa mtu aliyefanya Hajj ya Tamattu´ ambaye hakupata kichinjwa cha Hadiy. Hayo ni kutokana na yale yaliyopokelewa kutokamkwa Ibn ´Umar na ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambao wamesema:

“Haikuruhusiwa kufunga siku za Tashriyq isipokuwa kwa yule ambaye hakupata kichinjwa cha Hadiy.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy.

[1] al-Bukhaariy (1894) na tazama ”Fath-ul-Baariy” (4/243).

  • Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 15/05/2025