159 – Abu Bakr ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Idriys na Wakiy´ wametukhabarisha… ´Abdul-A´laa bin Hammaad an-Narsiy ametukhabarisha: Sufyaan ametukhabarisha: Ismaa´iyl bin Abiy Khaalid ametukhabarisha, kutoka kwa Qays bin Abiy Haazim, kutoka kwa al-Mustawrid, ndugu yake Banuu Fihr, ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Uhai wa dunia ukilinganisha na Aakhirah si vyengine isipokuwa ni kama mmoja wenu anayechovya kidole chake baharini; aone itarudi na nini.”[1]

160 – Muhammad bin Muslim bin Waarah ametuhadithia: Muhammad bin Sa´iyd bin Saabiq ametukhabarisha: ´Amr bin Abiy Qays ametukhabarisha, kutoka kwa Ibraahiym bin al-Muhaajir, kutoka kwa Qays bin Abiy Haazim, kutoka kwa al-Mustawrid mfano wa hayo.

[1] Muslim (2858).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 38 -39
  • Imechapishwa: 06/07/2025