26. Du´aa ya swalah ya Istikhaarah

74-

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رضي الله عنهما، قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُعَلِّمُنَا الِاسْتِخَارَةَ فِي الأُمُورِ كُلِّهَا، كَمَا يُعَلِّمُنَا السُّورَةَ مِنَ القُرْآنِ يَقُولُ: إِذَا هَمَّ أَحَدُكُمْ بِالأَمْرِ فَلْيَرْكَعْ رَكْعَتَيْنِ مِنْ غَيْرِ الفَرِيضَةِ، ثُمَّ لِيَقُلْ:

”Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kwa kusema:

”Mtume wa Allaah  alikuwa akitufundisha Istikhaarah katika mambo yote kama vile anavyotufunza Suurah ndani ya Qur-aan. Akisema: ”Mmoja wenu akikusudia kufanya jambo, basi aswali Rak´ah mbili zisizo za faradhi, kisha aseme:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْتَخِيرُكَ بِعِلْمِكَ، وَأَسْتَقْدِرُكَ بِقُدْرَتِكَ، وَأَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ العَظِيمِ، فَإِنَّكَ تَقْدِرُ وَلاَ أَقْدِرُ، وَتَعْلَمُ وَلاَ أَعْلَمُ، وَأَنْتَ عَلَّامُ الغُيُوبِ، اللَّهُمَّ إِنْ كُنْتَ تَعْلَمُ أَنَّ هَذَا الأَمْرَ خَيْرٌ لِي فِي دِينِي وَمَعَاشِي وَعَاقِبَةِ أَمْرِي – أَوْ قَالَ: عَاجِلِ أَمْرِي وَآجِلِهِ – فَاقْدُرْهُ لِي، وَيَسِّرْهُ لِي، ثُمَّ بَارِكْ لِي فِيهِ، وَإِنْ كُنْتَ تَعْلَمُ أَنَّ هَذَا الأَمْرَ شَرٌّ لِي فِي دِينِي وَمَعَاشِي وَعَاقِبَةِ أَمْرِي – أَوْ قَالَ عَاجِلِ وَآجِلِهِ – فَاصْرِفْهُ عَنِّي، وَاصْرِفْنِي عَنْهُ، وَاقْدُرْ لِي الخَيْرَ حَيْثُ كَانَ، ثُمَّ أَرْضِنِي به

”Ee Allaah! Hakika mimi nakutaka ushauri kwa ujuzi Wako na nakuomba uniwezeshe kwa uwezo Wako na nakuomba kutokana na fadhilah Zako tukufu. Hakika Wewe unaweza, nami siwezi, unajua, nami sijui Nawe ni mjuzi wa yaliyofichikana. Ee Allaah! Iwapo unajua kuwa jambo hili lina kheri nami katika dini yangu, maisha yangu na mwisho wa jambo langu” – au alisema: ”Duniani na Aakhirah” – basi nakuomba uniwezeshe nilipate na unifanyie wepesi kisha unibarikie kwacho. Endapo unajua kwamba jambo hili ni shari kwangu katika dini yangu, maisha yangu na mwisho wa jambo langu, basi liweke mbali nami, uniepushe nalo na nipangie jambo jengine lenye kheri nami popote lilipo, halafu niridhishe kwalo.”[1]

Hajuti yule mwenye kumtaka Allaah ushauri, akawashauri waja waumini na akawa imara katika jambo lake. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ ۖ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚإِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَوكِّلِينَ

”Washauri katika mambo na unapoazimia, basi mtegemee Allaah. Hakika Allaah anawapenda wanaotegemea.” [2]

[1] al-Bukhaariy (07/162) nambari (1162).

[2] 03:159

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 29/02/2020