26. Ambaye eti hajui kuwa manaswara wako katika batili na upotofu

Swali 26: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema:

“Mtu ikiwa hakuwakufurisha manaswara kwa sababu ya kutofikiwa na Aayah isemayo:

لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ

“Kwa hakika wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni watatu wa utatu.””[1]

basi hakufurishwi mpaka aijue Aayah hiyo?

Jibu: Hii inahitaji ufafanuzi zaidi. Ikiwa mtu huyo hajui kuwa manaswara wako katika batili, basi lazima hoja isimamishwe dhidi yake. Lakini ikiwa anajua wazi kwamba wao wako katika batili na kwamba amewakufurisha na anazijua dalili basi ni kafiri, kwa sababu atakuwa hakuwakufurisha washirikina.

[1] 05:73

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 58
  • Imechapishwa: 09/01/2026