al-´Ayyaashiy amesema kuhusu Kauli ya Allaah (Ta´ala):
فَتَلَقَّىٰ آدَمُ مِن رَّبِّهِ كَلِمَاتٍ فَتَابَ عَلَيْهِ
“[Kisha] Aadam akapokea maneno kutoka kwa Mola wake na [Mola Wake] Akapokea tawbah yake.” (02:37)
“Kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Kaathiyr amepokea kutoka kwa Abu ´Abdillaah ambaye amesema: “Wakati Allaah Alipochukua fungamano kwa Aadam basi akawa amemuonesha kizazi chake. Akamuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa amekaa na huku amemshegamia ´Aliy na baada yao amekaa Faatwimah na al-Hasan na al-Husayn wamekaa baada ya Faatwimah. Allaah Akasema: “Ee Aadam! Ninakutahadharisha kuwaangalia kwa hasadi. La sivyo nitakuteremsha kutoka pembezoni mwangu.” Baada ya Allaah kumwacha akaingia Peponi Akamuonyesha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ´Aliy, Faatwimah, al-Hasan na al-Husayn. Akawaangalia kwa hasadi. Baada ya hapo kukatambulishwa uongozi [wao] kwake, lakini akaukanusha na hivyo Pepo ikamrushia majani yake. Baada ya kutubu kwa Allaah kwa hasadi yake, kukubali uongozi na kuomba kwa haki ya watano – Muhammad, ´Aliy, Faatwimah, al-Hasan na al-Husayn – ndipo Allaah Akamsamehe. Hii ndio maana ya Kauli Yake:

Mhakiki ameelekeza hilo kwa “al-Bihaar” na “al-Burhaan”.
1- Allaah Amemtakasa Abu ´Abdillaah na uongo huu na upotoshaji wa Kitabu cha Allaah na uongo kwa Allaah ulio ndani yake na kumkufurisha Nabii wa Allaah Aadam kwa kupinga uongozi. Kwa mujibu wa Raafidhwah ni ukafiri kuupinga.
2- Aadam anatuhumiwa kuwa na hasadi kwa watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ni moja katika tabia ilio chafu kabisa.
3- Kujengea juu ya kisa hiki cha wapotevu hawa Baatwiniyyah Aadam alikufuru na kufanya hasadi kabla ya Shaytwaan.
4- Anaikadhibisha Qur-aan. Allaah Anasema kuwa dhambi ya Aadam na mke wake ilikuwa ni kula kwenye mti waliokatazwa kula. Shaytwaan akawashawishi wakala. Allaah (Ta´ala) Amesema:
وَقُلْنَا يَا آدَمُ اسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ وَكُلَا مِنْهَا رَغَدًا حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَـٰذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ فَأَزَلَّهُمَا الشَّيْطَانُ عَنْهَا فَأَخْرَجَهُمَا مِمَّا كَانَا فِيهِ ۖ وَقُلْنَا اهْبِطُوا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ وَلَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ فَتَلَقَّىٰ آدَمُ مِن رَّبِّهِ كَلِمَاتٍ فَتَابَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ
“Na Tukasema: “Ee Aadam! Kaa wewe na mkeo Pepo na kuleni humo maridhawa popote mpendapo na wala msiukaribie mti huu; mtakuwa miongoni mwa madhalimu!” Shaytwaan akawatelezesha wote wawili kwayo, Akawatoa kutoka katika hali waliyokuwa nayo. Tukasema: “Shukeni mkiwa maadui nyinyi kwa nyinyi, na mtapata katika ardhi makazi na starehe hadi muda maalum! Kisha Aadam akapokea maneno kutoka kwa Mola wake na [Mola wake] Akapokea tawbah yake – hakika Yeye Ndiye Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu.” (02:35-37)
وَيَا آدَمُ اسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ فَكُلَا مِنْ حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَـٰذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ فَوَسْوَسَ لَهُمَا الشَّيْطَانُ لِيُبْدِيَ لَهُمَا مَا وُورِيَ عَنْهُمَا مِن سَوْآتِهِمَا وَقَالَ مَا نَهَاكُمَا رَبُّكُمَا عَنْ هَـٰذِهِ الشَّجَرَةِ إِلَّا أَن تَكُونَا مَلَكَيْنِ أَوْ تَكُونَا مِنَ الْخَالِدِينَ وَقَاسَمَهُمَا إِنِّي لَكُمَا لَمِنَ النَّاصِحِينَ فَدَلَّاهُمَا بِغُرُورٍ ۚ فَلَمَّا ذَاقَا الشَّجَرَةَ بَدَتْ لَهُمَا سَوْآتُهُمَا وَطَفِقَا يَخْصِفَانِ عَلَيْهِمَا مِن وَرَقِ الْجَنَّةِ ۖ وَنَادَاهُمَا رَبُّهُمَا أَلَمْ أَنْهَكُمَا عَن تِلْكُمَا الشَّجَرَةِ وَأَقُل لَّكُمَا إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمَا عَدُوٌّ مُّبِينٌ قَالَا رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ قَالَ اهْبِطُوا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ وَلَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ
“Ee Aadam! Ishi wewe na mkeo Peponi na mle humo popote mpendapo na wala msikaribie mti huu, msijekuwa miongoni mwa madhalimu.” Basi shaytwaan akawatia wasiwasi ili kuwafichulia yaliyofichwa ya sehemu zao za siri. Na akasema: “Mola wenu Hakukukatazeni [kuukaribia] mti huu isipokuwa msijekuwa Malaika au kuwa miongoni mwa wenye kudumu.” Naye akawaapia [kwa kuwaambai]: “Hakika mimi kwenu ni mwenye kukunasihini kidhati.” Basi akawachota kwa [maneno ya] kupambia. Basi walipoonja mti ule zikawafichukia sehemu zao za siri na wakaanza kujibandika majani ya Pepo. Na Mola wao Akawaita [na kuwaambia]: “Je, kwani Mimi Sikukukatazeni mti huo na kukuambieni kwamba shaytwaan ni adui dhahiri kwenu?” Wakasema: “Mola wetu! Tumedhulumu nafsi zetu na basi Usipotusamehe na Ukaturehemu; bila shaka tutakuwa miongoni mwa waliokhasirika.” Akasema: “Shukeni! Nyinyi kwa nyinyi ni maadui. Na kwenye ardhi ndio itakuwa makazi na starehe mpaka muda [maalumu tu].” (07:19-24)
Aayah hizi zinaonyesha wazi kabisa ya kwamba dhambi ya Aadam na mke wake ilikuwa ni kula kwenye mti na ilikuwa ni kwa sababu ya njama za Shaytwaan na kuwavutia kwenye mti. Kadhalika zinaonyesha wazi waliyoyasema kuwambia Mola Wao, nayo ni:
رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ
“Mola wetu! Tumedhulumu nafsi zetu na basi Usipotusamehe na Ukaturehemu; bila shaka tutakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”
Hawakufanya Tawassul kwa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama wanavozusha hawa Baatwiniyyah.
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 58-59
- Imechapishwa: 19/03/2017

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 58-59
Imechapishwa: 19/03/2017
https://firqatunnajia.com/26-al-ayyaashiy-upotoshaji-wa-pili-wa-al-baqarah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)