Swali 257: Ni ipi hukumu ya wanawake kuyatembelea makaburi? Ni ipi hekima ya wanawake kukataliwa kuyatembelea makaburi?
Jibu: Mwanamke hana haki ya kuyatembelea makaburi. Maoni yenye nguvu kwa mujibu wa maono ya wanazuoni ni kwamba ni haramu kwake kuyatembelea makaburi. Bali ni katika madhambi makubwa. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallaam) amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi. Laana haiwi isipokuwa juu ya dhambi kubwa. Wanazuoni wamesema kuwa alama ya dhambi kubwa ni ile inayopelekea kulaaniwa. Laana ni adhabu kubwa ambayo haiwi isipokuwa ni kutokana tu na dhambi kubwa.
Lakini mwanamke akipita karibu na makaburi, hapana vibaya akasimama na akawaombea waliyomo ndani ya makaburi. Ama kukusudia kutoka nyumbani kwake kwa ajili ya kuenda kuyatembelea makaburi ndio jambo lililoharamishwa.
Hekima ya makatazo hayo ni kwamba kuna madhara mengi kwa mwanamke kuyatembelea makaburi. Mosi ni kwamba mwanamke ni kiumbe mwenye utashi dhaifu na mwenye hisia za karibu. Pengine asiweze wakati ataposimama karibu na kaburi la jamaa zake. Matokeo yake akaanza kulia, kuomboleza na kelele, mambo ambayo yanapelekea kwake kudhurika katika dini na mwili wake.
Pili ni kwamba makaburini mara nyingi zinakuwa ni sehemu ambazo hakuna watu. Kuna uwezekano watenda madhambi na wanaume wasio na maadili wakamshambulia maeneo kama hayo.
Tatu ni kwamba mwanamke anaweza kufanya kuyatembelea makaburi ikawa ndio kawaida yake, kwa sababu azimio yake ni dhaifu na ni mwenye hisia za haraka. Matokeo yake akaidhuru dini na dunia yake. Hivyo nafsi yake ikawa imefungamana na makaburi hayo.
Na kama kusingelikuwepo hekima nyingine zaidi ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi, basi hilo pekee lingetosha kwake kujihadhari na kitendo hicho. Kwa sababu Allaah (Ta´ala) au Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wanapohukumu jambo lolote, basi halina kheri yoyote kwetu:
وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا
“Haiwi kwa muumini mwanamme na wala kwa muumini mwanamke pindi Allaah anapohukumu na Mtume Wake jambo lolote iwe wana khiyari katika jambo lao – na yule anayemuasi Allaah na Mtume Wake, basi kwa hakika amepotoka upotofu wa wazi.”[1]
[1] 33:36
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/278-279)
- Imechapishwa: 28/02/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/278-279)
Imechapishwa: 28/02/2026
https://firqatunnajia.com/257-ni-ipi-hukumu-ya-wanawake-kuyatembelea-makaburi/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket