Swali 256: Ni ipi hukumu ya kuwatengenezea chakula wafiwa wa maiti kwa njia ya kwamba kila siku kuna watu maalum wanaojitolea kuwapikia chakula? Mara nyingi inakuwa ni kichinjwa kilichopikwa wanapewa. Hoja yao ni kwamba wafiwa wameshughulishwa kupika chakula.
Jibu: Kilichothibiti katika Sunnah ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema baada ya Ja´ar bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) kufa kama shahidi:
“Watengenezeeni chakula familia ya Ja´far! Hakika mambo yalivyo wamefikwa na kinachowashughulisha.”[1]
Lakini sio kwa njia inayofanywa na baadhi ya watu hii leo. Vichinjwa wanavyochinjiwa wafiwa wa maiti vinakuwa vingi na wanakikusanyikia watu wengi kukila. Jambo hilo halikuwekwa katika Shari´ah. Kule kushughulishwa kulikokuweko wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakupatikani hii leo. Kuna mikahawa mingi na karibu, khaswa katika miji. Kwa hivyo hawana haja ya kuwatengenezea chakula.
[1] Ahmad (6/266), Abu Daawuud (3132) na at-Tirmidhiy (998) aliyesema kuwa Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/281)
- Imechapishwa: 27/02/2026
Swali 256: Ni ipi hukumu ya kuwatengenezea chakula wafiwa wa maiti kwa njia ya kwamba kila siku kuna watu maalum wanaojitolea kuwapikia chakula? Mara nyingi inakuwa ni kichinjwa kilichopikwa wanapewa. Hoja yao ni kwamba wafiwa wameshughulishwa kupika chakula.
Jibu: Kilichothibiti katika Sunnah ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema baada ya Ja´ar bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) kufa kama shahidi:
“Watengenezeeni chakula familia ya Ja´far! Hakika mambo yalivyo wamefikwa na kinachowashughulisha.”[1]
Lakini sio kwa njia inayofanywa na baadhi ya watu hii leo. Vichinjwa wanavyochinjiwa wafiwa wa maiti vinakuwa vingi na wanakikusanyikia watu wengi kukila. Jambo hilo halikuwekwa katika Shari´ah. Kule kushughulishwa kulikokuweko wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakupatikani hii leo. Kuna mikahawa mingi na karibu, khaswa katika miji. Kwa hivyo hawana haja ya kuwatengenezea chakula.
[1] Ahmad (6/266), Abu Daawuud (3132) na at-Tirmidhiy (998) aliyesema kuwa Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/281)
Imechapishwa: 27/02/2026
https://firqatunnajia.com/256-ni-ipi-hukumu-ya-kuwatengenezea-chakula-wafiwa-wa-maiti/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket