Swali 255: Hivi karibuni kumeenea kwa ajabu suala la vyakula vya mchana na ubadhirifu kwa lengo kutaraji malipo na kuwaliwaza jamaa zake mfiwa. Unasemaje juu ya jambo hilo na sababu ya kuzidi kwake?
Jibu: Ndugu zake mfiwa kutengeneza chakula na kufanya chakula cha mchana ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah. Bali ni kwamba Jariyr bin ´Abdillaah al-Bajaliy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Tulikuwa tukizingatia kukusanyika kwa familia ya maiti na kutengeneza chakula baada ya mazishi ni aina fulani ya kuomboleza.”
Imethibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani mwanamke anayeomboleza na mwanamke anayesikiliza maombolezo.
Kuhusu maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Watengenezeeni chakula familia ya Ja´far! Hakika mambo yalivyo wamefikwa na kinachowashughulisha.”[1]
ni kwa sababu familia yake ilishughulishwa kutokana na kutengeneza chakula, na sio kwa sababu ya kuwaliwaza kwa chakula cha mchana. Jengine ni kuwa aliamrisha famila yake Ja´far ilitengenezewe chakula, kwa maana ya kwamba inakuwa kwa kiwango kinachowatosheleza watu wa pale nyumbani. Hilo linafahamisha kuwa amri yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilikuwa inatokana na haja na kwa kiasi cha haja yenyewe. Makusudio hayakuwa hayo yaliyotajwa katika swali. Watu wengi hii leo hawahitaji kuwatengenezea chakula. Kwa sababu nyumba nyingi hii za leo zimejaa vyakula vilivyokwishaandaliwa.
[1] Ahmad (6/266), Abu Daawuud (3132) na at-Tirmidhiy (998) aliyesema kuwa Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/280)
- Imechapishwa: 27/02/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/280)
Imechapishwa: 27/02/2026
https://firqatunnajia.com/255-ni-ipi-hukumu-ya-vyakula-vya-mchana-wakati-anapofariki-mtu/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket