Swali 254: Watu wameenda mbali zaidi inapokuja katika suala la rambirambi. Wakati watu wanapofiwa na mtu hukusanyika na wanamtengenezea chakula na wanamchinjia mnyama. Tunapowagusia hilo wanasema ´Tusiwape watu wanaokuja kututembelea chakula?` Tunawapogusia kuhusu watu kukaa kwa ajili ya kutoa mkono wa pole wanasema ´Ni wapi tutawapokea watu?`
Jibu: Rambirambi sio mapokezi kama mtu anavyompokea mgeni wake aliyefika. Rambirambi inahusiana na kwamba tunapomuona mtu ambaye amepatwa na msiba na ameathirika basi tunamzungumzisha kwa yale ambayo yatafanya kuuona mwepesi msiba wake. Haya ndio malengo ya rambirambi. Kwa mfano tunamwambia kama alivyopokea Usaamah bin Zayd:
“Tulikuwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati mmoja katika wasichana wake alipomtumia mjumbe kumweleza kuwa mtoto wake wa kiume ameaga dunia. Akamwambia yule mjumbe kwamba arejee kwake na amweleze:
أَنَّ لِلَّهِ مَا أَخَذَ، وَلَهُ مَا أَعْطَى، وَكُلُّ شَيْءٍ عِنْدَهُ بِأَجَلٍ مُسَمًّى، فَمُرْهَا فَلْتَصْبِرْ وَلْتَحْتَسِبْ
“Ni Chake Allaah kile alichokichukua na ni Chake alichokitoa na kila kitu Kwake kina muda maalum.”
Mwamrishe avute subira na taraji malipo.”[1]
Hakuna haja ya kukusanyika nyumbani. Kukusanyika nyumbani ni mambo yanaenda kinyume na yale waliyokuwemo Salaf. Imefikia mpaka Salaf kuona kwamba kukusanyika nyumbani kwa maiti na kutengeneza chakula ni katika maombolezo. Kuomboleza ni katika madhambi makubwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani mwanamke anayeomboleza na mwanamke anayesikiliza maombolezo[2]. Lakini tunaposikia mtu ambaye ameathirika kwa kufariki kwa ndugu yake, rafiki yake au mtu mwengine, basi tunajitahidi kuwasiliana naye na kuhimiza asubiri na ataraji malipo. Ama kitendo tu cha ndugu kuaga dunia watu wanakusanyika na pengine taa zikawashwa, kukaandaliwa viti, wakaletwa wasomaji wa Qur-aan na mfano wa hayo ni mambo yasiyojuzu. Si kitambo kirefu watu walikuwa hawafanyi kabisa mambo kama haya. Anafiwa mtu wanamzika na mambo kwisha. Na wanapoona kuwa jamaa zake wana mahuzuniko, wanampa pole na kurudi nyumbani. Baadaye ambaye anakutana naye sokoni au msikitini anampa mkono wa pole. Ama mikusanyiko hapana shaka kwamba ni Bid´ah na ni mambo yanayotakiwa kukatazwa. Inakuwa mibaya zaidi ikiwa itakuwa na maombolezo na wanawake. Wanafunzi wanapaswa kuwafunza watu mambo haya kabla mambo hayajaenda mbali zaidi.
[1] al-Bukhaariy (7377) na Muslim (923).
[2] Abu Daawuud (3127).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/278-279)
- Imechapishwa: 12/02/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/278-279)
Imechapishwa: 12/02/2026
https://firqatunnajia.com/254-mikusanyiko-kwa-familia-ya-wafiwa-baada-ya-mazishi-ni-bidah-inayotakiwa-kukaripiwa/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket