Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Nakuusieni kumcha Allaah (´Azza wa Jall) na kusikiliza na kutii hata kama mtatawaliwa na mtumwa. Hakika yule atakayeishi zaidi katika nyinyi basi atakuja kuona tofauti nyingi kabisa. Hivyo basi jilazimieni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu na wenye kuongoza baada yangu. Ziumeni kwa magego yenu. Ninakutahadharisheni na mambo ya kuzua, hakika kila kitachozuliwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”[1]
Wakati wa tofauti watu wanatakiwa kurejea katika uongofu wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wa makhaliyfah. Amewaeleza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba makhaliyfah hawa ni waongofu na ni wenye kuongoza. Uongofu huu unatakiwa kufuatwa. Amesema kuwa (Radhiya Allaahu ´anhum) ni waongofu na akawatakasa kutokamana na upotevu bila ya ujuzi na upotevu kwa ujuzi. Allaah awawie radhi! Kwa hiyo wao ni wachaji, waongofu na watakasifu. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewaelekeza wale wakweli na wenye nia safi katika ´Aqiydah yake na ya watu hawa waongofu (Radhiya Allaahu ´anhum) pindi mapote yatapotofautiana.
´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) ana fadhilah nyingi. Fadhilah za Maswahabah kwa jumla zimeandikwa kwenye vitabu vingi. Hakuna kitu chochote kinachozungumzia ´Aqiydah isipokuwa ndani yake kimetaja fadhila za Maswahabah. Vilevile kuna vitabu vilivyoandika mambo hayo ikiwa ni pamoja vilevile na:
1 – Fadhwaail-us-Swahaabah cha Imaam wa Ahl-us-Sunnah Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah).
2 – Ma´rifat-us-Swahaabah cha Abu Nu´aym.
3 – al-Iswaabah cha Ibn Hajar.
4 – al-Istiy´ab cha Ibn ´Abdil-Barr.
5 – Usd-ul-Ghaabah cha Ibn-ul-Athiyr.
Vitabu vyote hivi zinawazungumzia Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) ambavyo vimebainisha usuhuba na fadhilah zao. Allaah awawie radhi wote!
[1] Ahmad (4/287), Abuu Daawuud (4753), at-Tirmidhiy (2676) na Ibn Maajah (42). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Mishkaah” (131).
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qurrat-ul-´Aynayn bi Tawdhwiyh Ma´aaniy ´Aqiydat-ir-Raaziyayn, uk. 40-41
- Imechapishwa: 15/10/2016

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qurrat-ul-´Aynayn bi Tawdhwiyh Ma´aaniy ´Aqiydat-ir-Raaziyayn, uk. 40-41
Imechapishwa: 15/10/2016
https://firqatunnajia.com/25-uokovu-wakati-wa-kutokea-tofauti/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)