Vivyo hivyo kuhusu Qur-aaan Tukufu. Imeandikwa kwa kiarabu wazi. Wanaozungumzishwa wanaielewa. Dalili zake ziko wazi na maana zake ziko wazi. wanaozungumzishwa wanaielewa na kufahamu maana zake, khaswa lengo lake tukufu na mada yenye nguvu zaidi – kumpwekesha Allaah (‘Azza wa Jall).
Ni jambo linalotambulika ya kwamba Maswahabah waliisikia Qur-aan na Sunnah kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wakaisoma na wakaisoma wale waliokuja baada yao. Wanazuoni wamezungumza na kufafanua maana zake, wamezungumza na kufafanua maana ya Hadiyth, yale yanayohusiana na hukumu na yasiyohusiana na hukumu. Wameafikiana juu ya maana nyingi za Qur-aan na Hadiyth. Hawakuzozana isipokuwa tu kuhusu machache katika mengi, khaswa vile vizazzi vya kwanza; kutofautinaa kati yao ni kidogo sana ukilinganisha na yale waliyoafikiana juu yake. Kutofautiana kati ya wale waliokuja baada yao kulikuwa kukubwa zaidi. Kadiri muda ulivyopita ndivyo kuliongeka kutofautiana. Vizazi vya baadaye vilikuwa na tofauti nyingi zaidi kuliko vile vizazi vya wale wa awali.
Qur-aan ina maamrisho yaliyo wazi na yaliyojificha, na makatazo yaliyo wazi na yaliyojificha. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amebainisha viwango vya swalah, nyakati zake na sifa zake. Aidha amebainisha zakaah, kiwango chake cha wajibu kuitoa na viwango vyake. Vivyo hivyo kuhusu ´ibaadah nyingine zote. Mengi katika mambo haya ummah umeyanakili kwa mapokezi tele, kutoka kizazi hadi kizazi. Hivyo viumbe wakapata elimu ya lazima juu ya mambo hayo kama vile ambavyo wamepata elimu ya lazima ya kwamba amewafikishia matamshi yake, kwamba aliwapiga vita washirikina na Watu wa Kitabu, alipewa Utume akiwa Makkah, akahajiri Madiynah, akawalingamia ummah ya kwamba washuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki mwingine isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, akawakhabarisha ya kuwa Qur-aan hii ni maneno ya Allaah ambayo amezungumza nayo na si maneno yake yeye wala maneno ya kiumbe mwingine yeyote wala si maneno ya mtu, akawafunza ya kwamba Mola wao yuko juu ya mbingu Yake na juu ´Arshi Yake, kwamba Malaika huteremka kutoka Kwake kwenda Kwake na kisha wakapanda kwake tena, kwamba Mola wake anasikia, anaona, anazungumza, anaita kwa sauti, anapenda, anachukia, anaridhia, anakasirika, kwamba anyo mikono miwili na uso, anajua ya siri na yenye kujificha; hakifichiki Kwake chochote mbinguni wala ardhini, atawafufua kutoka makaburini mwao wakiwa hai baada ya kuteketea na kuwapeleka ima Peponi au Motoni[1].
[1] as-Sawaa´iq al-Mursalah (2/653-654) ya Ibn-ul-Qayyim.
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 44-45
- Imechapishwa: 30/11/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 44-45
Imechapishwa: 30/11/2025
https://firqatunnajia.com/25-ujumbe-wa-uislamu-uko-wazi-kabisa/