6- Sharti ya sita: Kumtakasia nia Allaah. Maana yake ni kukitakasa kitendo aina zote za taka za shirki kwa njia ya kwamba mtu asitamke hivo kwa kulenga pato lolote lile la kidunia, kutaka kuonekana wala kusikika. Hayo ni kutokana na yaliyokuja katika Hadiyth ya ´Utbaan ambaye amesema:
“Hakika Allaah ameuharamisha Moto kwa yule mwenye kusema ´Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah` hali ya kuwa anasema hivo kwa kutaka uso wa Allaah.”[1]
7- Sharti ya saba: Kuyapenda maneno haya, yale yenye kufahamishwa nalo, wenye nalo na wenye kufanyia kazi muqtadha yake. Amesema (Ta´ala):
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللّهِ أَندَاداً يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللّهِ
”Wapo katika watu ambao wanafanya badala ya Allaah washirika [na] wanawapenda kama mapenzi [yapasavyo] ya kumpenda Allaah.”[2]
Watu wenye neno “Laa ilaaha illa Allaah” wanampenda Allaah kikweli. Upande mwingine washirikina wanampenda Allaah na wanampenda pamoja Naye wengine, jambo ambalo linapingana na muqtadha ya “Laa ilaaha Allaah”.
[1] al-Bukhaariy (415) na Muslim (33).
[2] 02:165
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 50
- Imechapishwa: 19/02/2020
6- Sharti ya sita: Kumtakasia nia Allaah. Maana yake ni kukitakasa kitendo aina zote za taka za shirki kwa njia ya kwamba mtu asitamke hivo kwa kulenga pato lolote lile la kidunia, kutaka kuonekana wala kusikika. Hayo ni kutokana na yaliyokuja katika Hadiyth ya ´Utbaan ambaye amesema:
“Hakika Allaah ameuharamisha Moto kwa yule mwenye kusema ´Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah` hali ya kuwa anasema hivo kwa kutaka uso wa Allaah.”[1]
7- Sharti ya saba: Kuyapenda maneno haya, yale yenye kufahamishwa nalo, wenye nalo na wenye kufanyia kazi muqtadha yake. Amesema (Ta´ala):
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللّهِ أَندَاداً يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللّهِ
”Wapo katika watu ambao wanafanya badala ya Allaah washirika [na] wanawapenda kama mapenzi [yapasavyo] ya kumpenda Allaah.”[2]
Watu wenye neno “Laa ilaaha illa Allaah” wanampenda Allaah kikweli. Upande mwingine washirikina wanampenda Allaah na wanampenda pamoja Naye wengine, jambo ambalo linapingana na muqtadha ya “Laa ilaaha Allaah”.
[1] al-Bukhaariy (415) na Muslim (33).
[2] 02:165
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 50
Imechapishwa: 19/02/2020
https://firqatunnajia.com/25-sharti-ya-sita-na-ya-saba-ya-shahaadah-ikhlaasw-na-mapenzi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)