Miongoni mwa madhara ya kuacha kuswali kwa viatu ni kwamba baadhi ya waswaliji hukusanya viatu mahali pamoja, jambo ambalo linaweza kusababisha safu kutonyooka. Mosi safu zimeamrishwa kusawazishwa, pili kuna matishio kwa ambaye anasababisha safu kupinda. Tumeshuhudia safu zikivurugika katika uwanja wa Haram Makkah kwa sababu ya uwekwaji wa viatu, kwani watu walikosa nafasi ndani ya safu kutokana na wingi wa watu.
Madhara ya tatu ni kwamba wengi wa wanaoswali huacha kukagua viatu vyao kwenye milango ya misikiti kwa sababu hawakusudii kuswali navyo. Hili linaweza kusababisha uchafu kuingia msikitini kutoka katika viatu vyao na uchafu huo kuanguka msikitini. Haya yote ni matokeo ya kuacha Sunnah ya kukagua viatu mlangoni na kuvisafisha na mchanga ikiwa vina uchafu.
Madhara ya nne ni kwamba anayeswali huenda akaogopa viatu vyake kuibiwa na hivyo mawazo yake yakatatizika wakati wa swalah. Hili hufanya ukaondoka unyenyekevu, jambo ambalo ndio kiini cha swalah. Allaah (Ta´ala) amesema:
قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ
“Hakika wamefaulu waumini; ambao katika swalah zao ni wenye kunyenyekea.”[1]
Kuna Hadiyth zinazohimiza kuondoa kile kinachoweza kushawishi swalah ya mtu. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna swalah wakati chakula kichatengwa au mtu anaposhikwa na haja kubwa au ndogo.”[2]
Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Chakula kikitengwa, anzeni nacho kabla ya kuswali Maghrib. Msifanye haraka na chakula chenu cha jioni.”[3]
Aliyasema haya (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili kuchunga unyenyekevu.
[1] 23:01-02
[2] Muslim (560).
[3] al-Bukhaariy (672) na Muslim (557).
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 27-28
- Imechapishwa: 19/06/2025

Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 27-28
Imechapishwa: 19/06/2025
https://firqatunnajia.com/25-madhara-makubwa-ya-kuacha-kuswali-na-viatu/