Wanazuoni wamekhitilafiana kuhusu hukumu ya kuendelea kufunga bila kufuturu katika mitazamo mitatu:

1 – Kuunganisha swawm ni haramu. Haya ni maoni ya maimamu watatu; Abu Haniyfah, Maalik na ash-Shaafi’iy[1]. Ibn-ul-Mulaqqin ameegemeza maoni haya kwa kikosi kikubwa cha wanazuoni[2]. Ibn Hazm ameweka wazi juu ya uharamu wake[3]. Wamejengea hoja kwa dalili mbili:

Ya kwanza: Mantiki ya dhahiri ya katazo. Wamesema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuunganisha swawm na Maswahabah hakukuwa ni kuwahalalishia kitendo hicho bali ilikuwa ni kuwaadhibu, kwa sababu amesema:

”… kama mwenye kuwaadhibu.”

Yale ambayo yanafanywa kwa njia ya kuadhibu hayawi ni katika Shari´ah.

Ya pili: ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Usiku ukiingia kutoka upande huu na mchana ukaondoka kutoka upande huu na jua likazama, basi mwenye kufunga ameshafuturu.”[4]

Dalili kutoka Hadiyth hii ni kuwa Shari´ah haijafanya usiku kuwa mahali pa kitu kingine isipokuwa futari na mwisho wa swawm. Hivyo kuendelea kufunga kunakwenda kinyume na mpangilio huu, kama ilivyo siku ya ‘iyd ambapo hairuhusiwi kufunga.

[1] al-Istidhkaar” (10/153) na ”al-Majmuu’” (06/318).

[2] al-I´ilaam (05/326).

[3] al-Muhallaa (07/21).

[4] al-Bukhaariy (1954) na Muslim (1100).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/35-36)
  • Imechapishwa: 11/02/2025