09 – Wanawake kutoka kwa wingi kwenda sokoni

Miongoni mwa makosa yanayoenda kinyume na Shari´ah ni wanawake kutoka kwa wingi kwenda masokoni kwa sababu ya haja au pasi na haja. Bali anatoka akiwa amejipodoa kikamilifu kana kwamba ni  biharusi anayepelekwa kwa mume wake na anazungumza na wachuuzi kwa kujiachia kabisa. Bali baadhi ya wanawake wanafanya mzaha na mwenye duka, jambo ambalo lina khatari kubwa. Kwa hivyo hakikisha unamtuma mmoja katika ndugu zako wa kiume. Wasipojua unachohitaji basi toka ukiwa na ndugu yako asiyeweza kukuoa, kwani kufanya hivo ndio salama zaidi.

  • Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 29
  • Imechapishwa: 27/02/2026