105 – Abu Muhammad al-Hasan bin Ahmad al-Harbiy al-Khatwiyb amenikhabarisha: Ahmad bin Ja´far bin Hamdaan ametukhabarisha kwamba al-´Abbaas bin Yuusuf ash-Shakaliy amewadithia: Muhammad bin Maahaan ametuhadithia: Muhammad bin Yaziyd bin Khunays ametukhabarisha: Nimemsikia Wuhayb bin al-Ward akisema:

”Kulipigwa mfano wa mwanachuoni muovu kukasemwa: ”Mwanachuoni muovu ni kama jiwe lililoanguka kwenye gurudumu la maji; upande mmoja halinywi maji, upande mwingine linawazuia wengine kutokana na maji, hivyo miti ikapata uhai kutokana nalo. Laiti wanazuoni waovu wangeliwanasihi wanazuoni waovu wakasema ´enyi waja wa Allaah! Sikilizeni yale ambayo tunakuelezeni juu ya Mtume wenu na wema wenu walitoangulia, myafanyie kazi na wala msitazame matendo yetu yaliyofeli, kwa sababu sisi tumepewa mtihani`, basi wangelikuwa wamewatakia waja wa Allaah kheri. Lakini wanachotaka ni kuwaita waja wa Allaah kwenye matendo yao maovu na kuwaingiza wao pamoja nao.”

106 – Abul-Qaasim ´Aliy bin Muhammad bin ´Aliy al-Iyaadiy ametukhabarisha: Abu Bakr Muhammad bin ´Abdillaah bin Swaalih al-Abhariy ametukhabarisha: ´Uthmaan bin ´Aliy ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Muhammad ash-Shämiy ametukhabarisha: Ishaaq bin Muusa al-Answaariy ametukhabarisha: Nimemsikia Ibn ´Uyaynah akisema:

”´Iysaa (´alayhis-Salaam) amesema: ”Enyi wanazuoni waovu! Mmeweka ulimwengu juu ya vichwa vyenu na Aakhirah chini ya miguu yenu! Maneno yenu ni tiba na matendo yenu ni ugonjwa. Mfano wenu ni kama mti wa mlozi; unampendeza yule mwenye kuutazama na unamuua yule mwenye kuula.”

107 – al-Hasan bin ´Aliy al-Jawhariy ametukhabarisha: Muhammad bin ´Imraan bin Muusa al-Marzubaaniy ametukhabarisha: Ahmad bin Muhammad bin ´Iysaa al-Makkiy ametuhadithia: Muhammad bin al-Qaasim bin Khallaad ametuhadithia: ´Abdul-Ghafuur bin ´Abdil-´Aziyz ametukhabarisha, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Wahb bin Munabbih, aliyesimulia kuwa ´Iysaa bin Maryam (´alayhis-Salaam) amesema:

”Ole wenu, enyi waja wa dunia! Miale ya jua yenye kusambaa inamsaidia nini kipofu ilihali hawezi kuiona? Basi vivo hivyo mwanachuoni haimnufaishi kitu elimu yake nyingi endapo hatoifanyia matendo. Matunda ni mengi na si yote yanayonufaisha na kuliwa. Wanazuoni ni wengi ambao si wote nyinyi mnaonufaika na elimu zao.  Kwa ajili hiyo jihadharini na wanazuoni waongo, ambao wamevaa mavazi ya pamba, wanaoinamisha vichwa vyao na wanaangalia chini ya nyuso zao kama nzi. Maneno yao yanapingana na vitendo vyao. Ni nani achumaye zabibu katika miiba au tini kwenye michongoma? Basi vivyo hivyo maneno ya mwanachuoni mwongo hayazalishi kitu isipokuwa tu uwongo. Mmiliki ngamia asipomfunga ngamia wake nyikani, basi hukimbia mjini mwake. Mwanachuoni asipoifanyia kazi elimu yake, hutoka kifuani mwake, ikamwacha na kumkimbia. Mmea haukui isipokuwa kwa maji na udongo. Basi vivyo hivyo imani haikui isipokuwa kwa elimu na matendo. Ole wenu, enyi waja wa dunia! Hakika kila kitu kina alama tatu ambazo ima zinakuwa kwa ajili ya kitu hicho au dhidi yake. Dini ina alama tatu zinazoitambulisha: imani, elimu na matendo.

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 66-68
  • Imechapishwa: 13/05/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy