Haafidhw wa magharibi Abu ´Umar bin ´Abdil-Barr amesema alipokuwa akifafanua Hadiyth ya Ushukaji:
“Hadiyth hii imethibiti na cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. Ahl-ul-Hadiyth hawakukhilafiana juu ya usahihi wake. Imepokelewa kupitia njia nyingi na kwa namna nyingi. Ndani yake kuna dalili kuwa Allaah yuko mbinguni juu ya ‘Arshi Yake juu ya mbingu saba, kama walivyosema kikosi kikubwa cha wanazuoni. Hii ni miongoni mwa hoja zao dhidi ya Mu’tazilah, jambo ambalo linajulikana vyema kwa watu wa kawaida na wanazuoni. Aidha linafahamika vyema kuliko kuwa na haja ya kulielezea zaidi, kwa sababu ni jambo la dharurah ambalo hakuna yeyote aliyelijua kimaumbile wala hakuna muislamu yeyote aliyewakanusha juu ya hayo.”[1]
Akasema pia:
“Wanazuoni wa Maswahabah na wanafunzi wao, ambao tafsiri ya Qur-aan inachukuliwa kutoka kwao, wameafikiana juu ya tafsiri ya maneno Yake (´Azza wa Jall):
مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا
“Hauwi mnong’ono wa watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao, na wala watano isipokuwa Yeye ni wa sita wao, na wala chini kuliko ya hivyo na wala wengi zaidi isipokuwa Yeye yupamoja nao popote watakapokuwa, kisha siku ya Qiyaamah atawajulisha yale waliyoyatenda; hakika Allaah juu ya kila jambo ni mjuzi.”[2]
na akasema: ”Yeye yuko juu ya ´Arshi na ujuzi Wake uko kila mahali.” Hakuna yeyote anayetegemewa maneno yake ambaye alionelea kinyume.”[3]
Akasema tena:
“Ahl-us-Sunnah wamekubaliana kwa kauli moja kuhusu kukiri sifa zilizoelezwa ndani ya Qur-aan na Sunnah na kuzichukulia juu ya ukweli wake na si mafumbo. Isipokuwa hawakubainisha namna ya chochote katika hizo.
Ama Jahmiyyah, Mu’tazilah na Khawaarij wote wanazikanusha na hawakubali chochote kuwa ni cha ukweli. Wanadai kuwa yule anayezikubali ni mwenye kufananisha, ilihali wao kwa anayezithibitisha ni mwenye kumkanusha Muumba. Haki iko kwa wale ambao wananukuu Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – wao ni maimamu wa Mkusanyiko.”[4]
Haafidhw wa mashariki, Abu Bakr al-Khatwiyb amesema:
“Madhehebu ya Salaf ni kuthibitishasSifa na kuzipitisha juu ya dhahiri yake. Aidha kuzikanushia namna na ufananishaji.”
Vilevile al-Khattwaabiy amesema kabla yake. Mfano wa maneno kama haya yamesemwa na Imaam Abu al-Qaasim at-Taymiy wakati alipoulizwa kuhusu sifa za Muumba:
“´Aqiydah ya Maalik, ath-Thawriy, al-Awzaa’iy, ash-Shaafi’iy, Hammaad bin Salamah, Hammaad bin Zayd, Ahmad bin Hanbal, Yahyaa bin Sa’iyd, ´Abdur-Rahmaan bin Mahdiy, na Ishaaq bin Raahawayh ni kwamba sifa za Allaah alizojisifia nazo Yeye Mwenyewe na alizosifiwa na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama kusikia, kuona, uso, mikono na sifa nyinginezo ni juu ya maana zake za dhahiri zinazojulikana, bila ya kubainisha namna yoyote inayodhaniwa ndani yake, kufananisha wala kupindisha maana. Sufyaan bin ‘Uyaynah amesema:
“Kila kitu ambacho Allaah amejisifia nacho, basi kukisoma kwake ni tafsiri yake bila ya kukifanyia namna wala kukifananisha.
Kwa maana juu ya dhahiri yake. Haijuzu kukipindisha kwenda katika mafumbo kwa namna fulani ya yafsiri mbovu.”
[1] at-Tamhiyd (7/128-129).
[2] 58:7
[3] at-Tamhiyd (7/138-139).
[4] at-Tamhiyd (7/128).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 84-85
- Imechapishwa: 29/12/2025

Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 84-85
Imechapishwa: 29/12/2025
https://firqatunnajia.com/25-aqiydah-kutoka-mashariki-kwenda-magharibi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket