Inampasa pia ajipambe na adabu pamoja na wenzake na waliohudhuria katika kikao cha mwalimu, kwani kufanya hivo ni adabu kwa mwalimu na kulinda heshima ya kikao chake. Akae mbele ya mwalimu kwa kikao cha wanaojifunza, si kikao cha wanaofundisha. Wala asinyanyue sauti yake kwa juu sana bila haja, asicheke, asizidishe maneno bila haja, asicheze na mkono wake wala kitu kingine, asitazame kuliani wala kushotoni bila haja. Bali awe mwenye kumwelekea mwalimu huku akisikiliza maneno yake.
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 35
- Imechapishwa: 26/08/2026
Inampasa pia ajipambe na adabu pamoja na wenzake na waliohudhuria katika kikao cha mwalimu, kwani kufanya hivo ni adabu kwa mwalimu na kulinda heshima ya kikao chake. Akae mbele ya mwalimu kwa kikao cha wanaojifunza, si kikao cha wanaofundisha. Wala asinyanyue sauti yake kwa juu sana bila haja, asicheke, asizidishe maneno bila haja, asicheze na mkono wake wala kitu kingine, asitazame kuliani wala kushotoni bila haja. Bali awe mwenye kumwelekea mwalimu huku akisikiliza maneno yake.
Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 35
Imechapishwa: 26/08/2026
https://firqatunnajia.com/25-adabu-ya-mwanafunzi-katika-darsa/