Swali 249: Ni ipi hukumu ya kuswali na kufunga kwa ajili ya maiti?
Jibu: Kuna sampuli nne ya ´ibaadah zinazomfikia maiti kwa maafikiano:
1 – Du´aa.
2 – Mambo ya wajibu ambayo mtu anaweza kuweka naibu.
3 – Swadaqah.
4 – Kuacha mtumwa huru.
Mengine yote wanazuoni wametofautiana. Baadhi ya wanazuoni wanasema kuwa maiti hanufaiki kwa matendo mema anayozawadiwa yasiyokuwa haya manne. Lakini maoni ya sawa ni kwamba maiti ananufaika kwa matendo yote mema anayopewa muda wa kuwa maiti huyo ni muumini. Hata hivyo mimi sioni kuwa kumpa zawadi ya matendo mema maiti ni jambo lililowekwa katika Shari´ah ambalo mtu anatakwa kulifanya. Bali naona kuwa mtu anapompa maiti thawabu za matendo yoyote au akanuia thawabu za matendo fulani zimwendee maiti muislamu yanamfaa, lakini si jambo linalotakikana wala linalopendeza kwake. Dalili ya hilo ni kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwaamrisha ummah wake kufanya hivo. Bali imethibiti kwamba yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Anapofariki mwanadamu basi matendo yake hukatika isipokuwa mambo matatu; swadaqah yenye kuendelea, elimu ambayo watu wananufaika nayo au mtoto mwema mwenye kumuombea du´aa.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakusema “au mtoto mwema anayemfanyia matendo, kumfanyia ´ibaadah ya kumfungia, kumswalia na kadhalika”. Hapa kuna ishara ya kwamba kinachotakikana na ambacho kilichosuniwa ni kuwaombea du´aa wafu wetu, na sio kuwapa zawadi ya thawabu. Mtu mwenyewe ni mwenye kuhitajia matendo mema. Hivyo basi ajaalie matendo mema kwa ajili ya nafsi yake na akithirishe kuwaombea du´aa wafu wake. Hilo ndio bora zaidi na ndio matendo ya Salaf (Radhiya Allaahu ´anhum).
[1] Muslim (1631).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaan (17/255-256)
- Imechapishwa: 11/02/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaan (17/255-256)
Imechapishwa: 11/02/2026
https://firqatunnajia.com/249-ni-ipi-hukumu-ya-kuswali-na-kufunga-kwa-ajili-ya-maiti/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket