Swali 248: Je, swadaqah yenye kuendelea na mali inayotolewa inamfikia maiti?
Jibu: Tunapaswa kujua kuwa swadaqah yenye kuendelea inatakiwa iwe imeanzwa na yule maiti mwenyewe kabla ya kufa kwake. Mfano wake ni kama mtu ambaye amejenga msikiti. Hiyo ndio swadaqah yenye kuendelea. Mwengine amejitolea kama waqf kipoza maji. Mwengine amechimba kisima kwa ajili ya kuwanywesheleza watu. Hiyo ndio swadaqah yenye kuendelea. Mtu mwengine ametengeneza barabara ili iwe rahisi kwa watu kupita. Hiyo ni swadaqah yenye kuendelea.
Kuhusu swadaqah ambayo baadhi ya jamaa wanawatolea maiti, swadaqah hiyo inamfikia maiti, lakini sio alichokusudia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati aliposema:
“Anapofariki mwanadamu basi matendo yake hukatika isipokuwa mambo matatu; swadaqah yenye kuendelea, elimu ambayo watu wananufaika nayo au mtoto mwema mwenye kumuombea du´aa.”[1]
Hapa kunabakia suala moja kama ni bora kwa mtu kuwatolea swadaqah wazazi wake, kuwaswalia, kuwafungia au kuwaombea du´aa baada ya kuaga kwao dunia? Bora ni kuwaombea du´aa kwa sababu ya kufanyia kazi maelekezo yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Anapofariki mwanadamu basi matendo yake hukatika isipokuwa mambo matatu; swadaqah yenye kuendelea, elimu ambayo watu wananufaika nayo au mtoto mwema mwenye kumuombea du´aa.”
[1] Muslim (1631).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/254)
- Imechapishwa: 10/02/2026
Swali 248: Je, swadaqah yenye kuendelea na mali inayotolewa inamfikia maiti?
Jibu: Tunapaswa kujua kuwa swadaqah yenye kuendelea inatakiwa iwe imeanzwa na yule maiti mwenyewe kabla ya kufa kwake. Mfano wake ni kama mtu ambaye amejenga msikiti. Hiyo ndio swadaqah yenye kuendelea. Mwengine amejitolea kama waqf kipoza maji. Mwengine amechimba kisima kwa ajili ya kuwanywesheleza watu. Hiyo ndio swadaqah yenye kuendelea. Mtu mwengine ametengeneza barabara ili iwe rahisi kwa watu kupita. Hiyo ni swadaqah yenye kuendelea.
Kuhusu swadaqah ambayo baadhi ya jamaa wanawatolea maiti, swadaqah hiyo inamfikia maiti, lakini sio alichokusudia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati aliposema:
“Anapofariki mwanadamu basi matendo yake hukatika isipokuwa mambo matatu; swadaqah yenye kuendelea, elimu ambayo watu wananufaika nayo au mtoto mwema mwenye kumuombea du´aa.”[1]
Hapa kunabakia suala moja kama ni bora kwa mtu kuwatolea swadaqah wazazi wake, kuwaswalia, kuwafungia au kuwaombea du´aa baada ya kuaga kwao dunia? Bora ni kuwaombea du´aa kwa sababu ya kufanyia kazi maelekezo yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Anapofariki mwanadamu basi matendo yake hukatika isipokuwa mambo matatu; swadaqah yenye kuendelea, elimu ambayo watu wananufaika nayo au mtoto mwema mwenye kumuombea du´aa.”
[1] Muslim (1631).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/254)
Imechapishwa: 10/02/2026
https://firqatunnajia.com/248-je-swadaqah-yenye-kuendelea-na-mali-inayotolewa-inamfikia-maiti/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket