Swali 246: Ni upi usahihi wa Hadiyth inayosema:
“Katika kuwatendea wema wazazi baada ya kufa kwao ni wewe kuwaswalia wakati wa kuswali kwako na kuwafungia wakati wa kufunga kwao.”[1]?
Jibu: Hadiyth hii haikusihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini katika kuwatendea wema wazazi baada ya kufa kwako ni wewe kuwaombea msamaha, kuwaombea du´aa kwa Allaah, kuwakirimu marafiki zao, kuwaunga marafiki zao na kuwaunga jamaa ambao wana mafungamano baina yako wewe na wao. Huku ni katika kuwatendea wema wazazi baada ya kufa kwao. Kuhusu kuwaswalia swalah inayotambulika kwa mujibu wa Shari´ah au kuwafungia ni jambo halina msingi wowote.
[1] al-Muswannaf (3/387) kupitia kwa Ibn Abiy Shaybah.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/252)
- Imechapishwa: 09/02/2026
Swali 246: Ni upi usahihi wa Hadiyth inayosema:
“Katika kuwatendea wema wazazi baada ya kufa kwao ni wewe kuwaswalia wakati wa kuswali kwako na kuwafungia wakati wa kufunga kwao.”[1]?
Jibu: Hadiyth hii haikusihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini katika kuwatendea wema wazazi baada ya kufa kwako ni wewe kuwaombea msamaha, kuwaombea du´aa kwa Allaah, kuwakirimu marafiki zao, kuwaunga marafiki zao na kuwaunga jamaa ambao wana mafungamano baina yako wewe na wao. Huku ni katika kuwatendea wema wazazi baada ya kufa kwao. Kuhusu kuwaswalia swalah inayotambulika kwa mujibu wa Shari´ah au kuwafungia ni jambo halina msingi wowote.
[1] al-Muswannaf (3/387) kupitia kwa Ibn Abiy Shaybah.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/252)
Imechapishwa: 09/02/2026
https://firqatunnajia.com/246-ni-vipi-mtu-anawatendea-wema-wazazi-baada-ya-kufa-kwao/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket