Swali 242: Kuna ambao wanachinja ndani ya Ramadhaan na wanaita kuwa ni “Chakula cha jioni cha wazazi wawili”. Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Kuwatolea swadaqah wazazi wawili ni jambo linalofaa. Hapana vibaya. Hata hivyo kuwaombea du´aa ni bora kuliko kuwatolea swadaqah. Kwa sababu hilo ndilo ambalo amelikokoteza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akalihimiza pale aliposema:
“Anapofariki mwanadamu basi matendo yake hukatika isipokuwa mambo matatu; swadaqah yenye kuendelea, elimu ambayo watu wananufaika nayo au mtoto mwema mwenye kumuombea du´aa.”[1]
Hakusema “mtoto mwema anayemtolea swadaqah au anayemswalia”. Lakini akiwatolea swadaqah wafu wake itafaa. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa juu ya hilo akalijuzisha.
Hata hivyo yale yanayofanywa na baadhi ya watu katika kupanga masherehe mengi katika nyusiku za Ramadhaan ambayo hayahudhuriwi isipokuwa tu na matajiri ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah. Salaf hawakufanya hivo. Kwa ajili hiyo mtu anatakiwa asifanye hivo. Ukweli wa mambo ni kwamba, hata kama ni chakula tu ambacho kinakuja kuliwa na watu… ingawa wako baadhi ya watu ambao wanajikurubisha kwa Allaah kwa kuchinja na wanaona kwamba kufanya hivo ni bora kuliko kununua nyama, jambo ambalo linapingana na Shari´ah. Kwa sababu kichinjwa ambacho mtu anajikurubisha nacho kwa Allaah ni kichinjwa wakati wa Udhhiyah, wakati wa hijjah na ´Aqiyqah. Kujikurubisha kwa Allaah kwa kuchinja ndani ya Ramadhaan sio katika Sunnah.
[1] Muslim (1631).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/247)
- Imechapishwa: 05/02/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/247)
Imechapishwa: 05/02/2026
https://firqatunnajia.com/242-ni-ipi-hukumu-ya-kuwachinjia-wafu-ndani-ya-ramadhaan/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket