Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
175 – Tunamuomba atukinge kutokana na matamanio yanayotofautiana, fikira zinazotofautiana na madhehebu mabaya kama mfano wa Mushabbihah, Mu´tazilah, Jahmiyyah, Jabriyyah, Qadariyyah na wengine wote ambao wanaenda kinyume na Sunnah na mkusanyiko na wakakumbatia upotofu.
MAELEZO
Hakuna kingine kilichowafanya watu kupotea isipokuwa upotofu. Allaah (Subhaanah) amesema:
وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّنِ اتَّبَعَ هَوَاهُ بِغَيْرِ هُدًى مِّنَ اللَّـهِ
”Na nani mpotofu zaidi kuliko yule aliyefuata matamanio yake pasi na uongofu kutoka kwa Allaah?”[1]
أَفَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَـٰهَهُ هَوَاهَُ
“Je, umemuona yule aliyejifanyia matamanio yake kuwa ndio mungu wake?”[2]
Mtu anatakiwa kumuomba Allaah amsalimishe kutokana na matamanio na amwongoze katika haki, ijapo haki hiyo itapingana na matamanio yake. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَقَفَّيْنَا مِن بَعْدِهِ بِالرُّسُلِ ۖ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ ۗ أَفَكُلَّمَا جَاءَكُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَىٰ أَنفُسُكُمُ اسْتَكْبَرْتُمْ فَفَرِيقًا كَذَّبْتُمْ وَفَرِيقًا تَقْتُلُونَ
“Hakika Tulimpa Muusa Kitabu na tukafuatisha baada yake Mitume na Tukampa ‘Iysaa, mwana wa Maryam, hoja za wazi na tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu. Je, basi kila anapokujieni Mtume kwa yale yasiyoyapenda nafsi zenu, basi mlitakabari, hivyo kundi [katika nyinyi] mlilikadhibisha na kundi [jengine] mnaliua.”[3]
Matamanio ni khatari mno.
Hayo yaliyotangulia ndio yale mapote ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza juu yake pale aliposema:
“Ummah huu utafarikiana makundi sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.” Wakasema: “Ni lipi hilo, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni wale wataofuata yale ninayofuata mimi hii leo na Maswahabah wangu.”[4]
Kwa sababu yameiacha haki. Kundi pekee lililosalimika ni lile ambalo linafuata yale yaliyokuwa yakifuatwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Hao ndio waliookoka kutokana na Moto, kwa ajili hiyo wakaitwa Kundi lililookoka. Madhehebu kikusudiwacho ni mitazamo na maoni mbalimbali.
[1] 28:50
[2] 45:23
[3] 2:87
[4] Ibn Maajah (3992), at-Tirmidhiy (2641) na Abu Daawuud (4596). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Mishkaat-ul-Maswaabiyh” (171).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 263-264
- Imechapishwa: 27/05/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 263-264
Imechapishwa: 27/05/2025
https://firqatunnajia.com/241-matamanio-ndio-yamewapotosha-watu/