241. Je, thawabu za kichinjwa cha Udhhiyah kinamfikia maiti ikiwa kimenunuliwa na pesa zisizokuwa zake?

Swali 241: Je, thawabu za kichinjwa cha Udhhiyah kinamfikia maiti ikiwa kimenunuliwa na pesa zisizokuwa zake? Kwa mfano kimenunuliwa na pesa za mtoto wake.

Jibu: Maoni sahihi ni kwamba analipwa thawabu kwa hilo. Hata hivyo sio katika Sunnah kumchinjia Udhhiyah maiti ikiwa hakuacha anausia jambo hilo. Lakini kama unataka kujichinjia Udhhiyah kutoka katika pesa zako basi chinja kwa ajili yako mwenyewe na kwa ajili ya familia yako. Na ukinuia kuwajumuisha watu basi hapana vibaya.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/246-247)
  • Imechapishwa: 04/02/2026