163 – Abul-Ahwasw Muhammad bin Hayyaan ametuhadithia: ´Affaan bin Muslim amenihadithia: ´Abdul-Waarith bin Sa´iyd ametukhabarisha: Abut-Tayyaah ametukhabarisha: Anas bin Maalik ametuhadithia:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa miongoni mwa watu bora zaidi kwa tabia njema.”[1]

164 – Ahmad bin Muhammad bin Ayyuub ametuhadithia: Ibraahiym bin Sa´d ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin Ishaaq, kutoka kwa Mu´aawiyah bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa ´Atwaa’ bin Abiy Rabaah, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Umar, ambaye ameeleza:

”Kulisemwa: ”Ee Mtume wa Allaah, ni yupi katika waumini aliye bora zaidi?” Akasema: ”Ni yule aliye bora zaidi katika tabia njema.”[2]

165 – az-Zubayr bin Abiy Bakr az-Zubayriy ametuhadithia: Abu Dhwamrah amenihadithia, kutoka kwa Naafiy´ bin ´Abdillaah, kutoka kwa Farwah bin Qays, kutoka kwa ´Atwaa’ bin Abiy Rabaah, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Umar, ambaye ameeleza:

”Kulisemwa: ”Ee Mtume wa Allaah, ni yupi katika waumini aliye bora zaidi?” Akasema: ”Ni yule aliye bora zaidi katika tabia njema.”

166 – Ahmad bin Maniy´ ametuhadithia: Haashim bin al-Qaasim ametuhadithia: Layth bin Sa´d ametuhadithia, kutoka kwa Yaziyd bin ´Abdillaah bin Usaamah, kutoka kwa ´Amr bin Abiy ´Amr, kutoka kwa al-Muttwalib, kutoka kwa ´Aaishah, ambaye ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah Allaah  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakika muumini kwa tabia njema hufikia daraja ya anayesimama usiku kwa ´ibaadah na kufunga mchana.”[3]

167 – Muhammad bin al-Husayn amenihadithia: Muhammad bin al-Qaasim al-Asdiy ametukhabarisha: ´Abdullaah bin ´Umar al-´Umariy ametuhadithia, kutoka kwa Naafiy´, kutoka kwa Ibn ´Umar, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakika mtu hufikia kwa tabia njema daraja ya anayesimama usiku kufanya ´ibaadah na kufunga kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall).”[4]

168 – Humayd an-Nasaa’iy ametuhadithia: Abul-Aswad an-Nadhwr bin ´Abdil-Jabbaar amenihadithia: Nuuh bin ´Abbaad al-Qurashiy – ambaye sijawahi kumuona mtu ambaye anamcha Allaah zaidi kuliko yeye – amenihadithia, kutoka kwa Thaabit al-Bunaaniy, kutoka kwa Anas bin Maalik, ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakika mja hufikia kwa tabia njema daraja kubwa za Aakhirah na heshima za makazi, hali yeye ni dhaifu wa ´ibaadah, na hakika hufikia kwa tabia mbaya daraja la chini zaidi katika Jahannam, hali yeye ni mfanya ´ibaadah.”[5]

169 – Abu Muhammad al-´Abbaas bin Abiy Twaalib al-Waasitwiy – mmoja katika ndugu zake wawili wa Yahyaa bin Abiy Twaalib – amenihadithia: ´Ubaydah bin Ishaaq ametuhadithia: Sinaan bin Haaruun ametuhadithia, kutoka kwa Humayd at-Twawiyl, kutoka kwa Anas, ambaye amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Tabia njema imekusanya kheri ya dunia na Aakhirah.”[6]

[1] al-Bukhaariy (6203) na Muslim (2150).

[2] Ibn Maajah (4259). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (3454).

[3] Abu Daawuud (4798). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (4798).

[4] al-Haakim (1/60), ambaye ameisahihisha Hadiyth kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.

[5] Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (1591).

[6] Dhaifu na inayopingana na zilizo Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (1604).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 205-216
  • Imechapishwa: 24/03/2026