101 – al-Hasan bin Abiy Bakr ametukhabarisha: Abu Sahl Ahmad bin Muhammad bin ´Abdillaah bin Ziyaad al-Qattwaan ametuzindua: Muhammad bin Ghaalib bin Harb ametuhadithia: Bishr bin ´Ubayd ad-Daarisiy ametuhadithia: Muhammad bin Sulaym ametuhadithia, kutoka kwa ´Atwaa’ bin as-Saa-ib, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Yaziyd, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Hudhayfah: Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”Mwenye kutafuta elimu kwa ajili ya kujifakharisha na wanazuoni, kuvutana na wapumbavu au kutaka nyuso za watu wamtazame yeye, basi atapata Moto kwa sababu ya elimu yake.”[1]

102 – Abul-Hasan ´Aliy bin ´Abdil-´Aziyz at-Twaahiriy ametukhabarisha: Abu Bahr Muhammad bin al-Hasan bin Kawthar ametuzindua: Muhammad bin Yuunus ametuhadithia: Abu Yuusuf Ya´quub bin al-Qaasim at-Twalhiy ametuhadithia: ´Uthmaan bin Matwar ametuhadithia: Abu Haashim ar-Rimaaniy ametuhadithia, kutoka kwa Anas bin Maalik: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwenye kutafuta elimu kwa ajili ya kutaka kuvutana na wapumbavu, kujionyesha kwa wanazuoni au kutaka nyuso za watu wamtazame yeye, basi ajiandalie makazi yake Motoni.”[2]

103 – Abul-Hasan Muhammad bin Ahmad bin Rizq ametukhabarisha: Abu ´Umar az-Zaahid Muhammad bin ´Abdil-Waahid ametukhabarisha: Ahmad bin Ziyaad al-Bazzaar ametuhadithia: Shurayj bin an-Nu´maan ametuhadithia: Fulayh – yaani Ibn Sulaymaan – ametuhadithia, kutoka kwa Abu Twuwaalah, kutoka kwa Sa´iyd bin Yasaar, kutoka kwa Abu Hurayrah: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwenye kujifunza elimu na si kwa jengine isipokuwa tu kwa sababu ya lengo la kidunia, basi hatonusa harufu ya Pepo.”[3]

Bi maana elimu inayotafutwa kwa ajili ya Allaah.

104 – Abu Bakr Muhammad bin ´Abdil-Malik bin Muhammad bin ´Abdillaah bin Bishraan al-Qurashiy amenikhabarisha: Abul-Fadhwl ´Ubaydullaah bin ´Abdir-Rahmaan az-Zuhriy ametuzindua… ´Aliy bin al-Muhsin at-Tannuukhiy pia ametuzindua: ´Abdullaah bin Ahmad bin Maahibazd al-Aswbahaaniy ametuhadithia: Ahmad bin ´Abdillaah bin Shaabuur ametuhadithia: Abu Nu´aym al-Halabiy ametuhadithia: Makhlad bin al-Husayn ametuhadithia: Hishaam bin Hassaan ametuhadithia: Nimemsikia al-Hasan akisema:

”Mwenye kutafuta elimu kwa ajili ya kutafuta Aakhirah, ataipata. Na mwenye kutafuta elimu kwa ajili ya kutafuta dunia, atapata fungu lake.”

az-Zuhriy amesema:

”Hilo ndio fungu lake.”

[1] Cheni yake ya wapokezi ni dhaifu mno kwa sababu ya ad-Daarisiy. Ibn ´Adiy amesema:

”Hadiyth zake kutoka kwa maimamu ni dhaifu na zinazopingana na zilizo Swahiyh. Unyonge wake uko wazi sana.”

al-Azdiy amemtuhumu uwongo.

[2] Cheni yake ya wapokezi ni dhaifu kwa sababu ya ´Uthmaan bin Matwar. adh-Dhahabiy amesema katika ”adh-Dhwu´afaa´”:

”Wamemdhoofisha.”

[3] Swahiyh, Ahmad (02/338) ameipokea na akasema: Yuunus na Surayj bin an-Nu´maan wametuhadithia: Fulayh ametuhadithia. Abu Daawuud, Ibn Maajah, Ibn Hibbaan, al-Haakim na Ibn ´Abdil-Barr katika “al-Jaami´” ameipokea kupitia njia zingine kutoka kwa Fulayh. al-Haakim amesema kuwa ni “Swahiyh kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim” na adh-Dhahabiy akaafikiana naye, mambo ni kama walivosema. Hata kama al-Bukhaariy na Muslim wamesimulia kutoka kwa Fulayh katika yale mapokezi ya kwanza, kulikuwepo unyonge katika kumbukumbu yake. Hata hivyo Hadiyth imefanyiwa ufuatiliaji na Ibn ´Abdil-Barr na inatiliwa nguvu na Hadiyth ya Anas ilio kabla yake. Inatiwa nguvu na Hadiyth zingine katika “at-Targhiyb wat-Tarhiyb”.

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 64-66
  • Imechapishwa: 13/05/2024
  • Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy