Masimulizi haya matukufu yamebeba sentesi nne:
1 – Kulingana juu si kitu kisichotambulika.
2 – Namna haifahamiki.
3 – Ni wajibu kuamini jambo hilo.
4 – Kuuliza juu yake ni Bid´ah.
Ni jumla zenye maana sahihi na majulisho matukufu. Kila jumla katika hizo ina dalili nyingi ndani ya Qur-aan na Sunnah, kama tutakavyoona karibuni. Hebu wacha tusimame katika kila sentensi ili kutaja dalili zake ndani ya Qur-aan na Sunnah.
1 – Kusema kwake kwamba kulingana juu si kitu kisichotambulika. Makusudio ni kwamba kulingana juu maana yake inafahamika. Kwa sababu Allaah ametuzungumzisha ndani ya Qur-aan Tukufu kwa lugha ya kiarabu kilicho wazi. Amesema (Ta´ala):
وَإِنَّهُ لَتَنزِيلُ رَبِّ الْعَالَمِينَ نَزَلَ بِهِ الرُّوحُ الْأَمِينُ عَلَى قَلْبِكَ لِتَكُونَ مِنَ الْمُنذِرِينَ بِلِسَانٍ عَرَبِيٍّ مُّبِينٍ
“Hakika huu ni uteremsho wa Mola wa walimwengu; ameuteremsha roho mwaminifu [na kuiingiza] kwenye moyo wako ili uwe miongoni mwa waonyaji kwa lugha ya kiarabu ilio wazi.”[1]
إِنَّا أَنزَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ
”Hakika Sisi tumekiteremsha kikisomeka kwa kiarabu ili mpate kufahamu.”[2]
كِتَابٌ فُصِّلَتْ آيَاتُهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لِّقَوْمٍ يَعْلَمُونَ
”Kitabu kilichopambuliwa waziwazi Aayah zake kikisomeka kwa kiarabu kwa watu wanaotambua.”[3]
وَهَـٰذَا كِتَابٌ مُّصَدِّقٌ لِّسَانًا عَرَبِيًّا
”… na hiki Kitabu kinasadikisha kwa lugha ya kiarabu… ”[4]
قُرْآنًا عَرَبِيًّا غَيْرَ ذِي عِوَجٍ لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ
”… Qur-aan ya kiarabu isiyo na kombo ili wapate kumcha Allaah.”[5]
Kwa hivyo Yeye (Subhaanah) ameiteremesha Qur-aan Tukufu kwa kiarabu kilicho wazi, kwa sababu “kiarabu ni lugha fasaha zaidi, iliyo wazi zaidi, ya ndani zaidi na yenye maana zaidi. Ndio maana Kitabu kitukufu kikateremshwa kwa lugha tukufu”[6]. Sababu nyingine ni kwamba wale wazungumzishwa waweze kuyaelewa maneno ya Allaah, kuyafahamu mazungumzisho Yake na kuelewa maana yake. Kama alivyosema (Ta’ala):
وَلَوْ جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا أَعْجَمِيًّا لَّقَالُوا لَوْلَا فُصِّلَتْ آيَاتُهُ ۖ أَأَعْجَمِيٌّ وَعَرَبِيٌّ
”Lau Tungekifanya kisomeke kwa lugha isiyokuwa ya kiarabu wangelisema: ”Mbona hazikupambanuliwa waziwazi Aayah zake?” Kwa lugha ya kigeni na hali ya kuwa ni mwarabu!”[7]
Miongoni mwa fadhilah za Allaah kwa viumbe vyake ni pamoja na kuwajaalia Mitume wanaozungumza lugha zao ili waweze kuelewa ujumbe wao. Amesema (Ta’ala):
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوْمِهِ لِيُبَيِّنَ لَهُمْ ۖ فَيُضِلُّ اللَّـهُ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ
”Hatukutuma Mtume yeyote isipokuwa kwa lugha ya watu wake ili awabainishie. Hivyo Allaah humpotoa amtakaye na humwongoza amtakaye. Naye ni Mwenye nguvu Asiyeshindika, Mwenye hekima.”[8]
Abu Dharr (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
”Allaah (´Azza wa Jall) hajapatapo kumtuma Mtume isipokuwa alikuwa akizungumza lugha ya watu wake.”[9]
[1] 26:192-195
[2] 12:02
[3] 41:3
[4] 46:12
[5] 39:28
[6] Tafsiyr-ul-Qur-aan al-´Adhwiym (4/294).
[7] 41:44
[8] 14:4
[9] Ahmad (5/158). al-Haythamiy amesema:
“Wasimulizi wake ni wanaume Swahiyh. Hata hivyo Mujaahid hakusikia chochote kutoka kwa Abu Dharr.” (Majma´-uz-Zawaa-id (7/43))
Hadiyth inatiliwa nguvu na Qur-aan.
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 43-44
- Imechapishwa: 30/11/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 43-44
Imechapishwa: 30/11/2025
https://firqatunnajia.com/24-kulingana-juu-si-kitu-kisichotambulika/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket